Wizara ya afya imedhibitisha kurekodi visa 5 vipya vya maambukizi ya virusi vya Mpox kufikia Jumanne Disemba 10, 2024. Idadi hiyo sasa imefikia maambukizi 28 katika kaunti 12 ambazo zimerekodi maambukizi hayo ya Mpox.
Katika visa vipya ambavyo vimerekodiwa wiki hii, visa 3 vimepatikana katika kaunti ya Nakuru huku kaunti ya Mombasa ikirekodi visa 2. Kwenye taarifa ya wizara ya afya iliyotiwa sahihi na waziri Deborah Barasa, wagonjwa 8 wako katika uangalizi wa daktari huku watu wengine 17 waliokuwa wameambukizwa wakiwa wamepona kikamilifu. Vile vile, wagonjwa wawili wapokatika karantini wakati mgonjwa mmoja aliaga dunia.
Katika kaunti zilizorekodi viruisi vya Mpox, Nakuru inaongoza kwa visa 9, Mombasa 6 huku Kajiado, Bungoma na Nairobi zikiwa na visa 2 kila mmoja. Kisa kimoja kimerekodiwa katika kaunti za Busia, Kiambu, Taita Taveta, Makueni, Kericho, Uasin Gixhu na Kilifi.
Hata hivyo wizara ya afya imesema kwamba inendelea kuzihusisha serikali za kaunti na washikadau wengine mbali mbali katika kuhamasisha umma na kusisitiza unuhimu wa wananchi kuchukua tahadhari za kujikinga dhidi ya Mpox. Wizara hiyo vile vile imesema kwamba inazidi kufuatilia na kuangazia mripuko wa virusi vya Mpox kote nchini.
Kufikia sasa tangu virusi hivo kuripotiwa nchini mwezi
Julai, wizara ya afya imeripoti kwamba jumlaya wasafiri 2,207,715 wamefanyiwa
vipimo katika sehemu za mbali mbali za mipaka za kuingia nchini.
Aidha visa 28 ambavyo vimedhibitikshwa na
mahabara ya humu nchini tangu Julai, vimetokana na sampuli 322 zilizowasilishwa
kwenye mahabara kufanyiwa uchunguzi. Majibu ya sampuli 2 zingali kutolewa.