logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Raila kujadiliana na wagombea wenzake wawili wa uenyekiti wa tume ya umoja wa Afrika

Mdahalo wa wagombea wa tume ya umoja wa Afrika kufanyika Addis Ababa nchini Ethiopia kwenye makao makuu ya Umoja wa Afrika

image
na OTIENO TONNY

Yanayojiri13 December 2024 - 12:51

Muhtasari


  • Mgombea wa nafasi ya uenyekiti wa tume ya Umoja wa Afrika kutoka nchini Kenya Raila Odinga amesema yuko tayari kukabiliana na washindani wake wakati wa mdahalo
  • Mdahalo huo kwa jina  ‘Mjadala Afrika’   utawasilishwa kwa lugha sita rasmi za muungano wa Afrika ikiwemo Kiingereza, Kifaransa, Kiarabu, Kireno, Kihispania na Kiswahili.


Mgombea wa nafasi ya uenyekiti wa tume ya Umoja wa Afrika kutoka nchini Kenya Raila Odinga amesema yuko tayari kukabiliana na washindani wake wakati wa mdahalo utakayopeperushwa  moja kwa moja kwenye mitandao mbali mbali na runinga kote Afrika  mnamo Ijumaa Disemba 13, 2024   kuanzia saa moja jioni majira ya Afrika Mashariki.

Raila anatarajiwa kueleza sera na suluhisho anazopania kutumia katika kukabili changamoto zinazoikumba bara la Afrika wakati wa mdahalo huo.

Mjadala huo utafanywa mbele ya hadhira ya moja kwa moja inayojumuisha wajumbe wa baraza kuu la tume ya umoja wa Afrika, wajumbe wa Kamati ya wawakilishi wa kudumu (PRC), Makamishna wa tume ya umoja wa Afrika , wawakilishi wa vyombo vya habari pamoja na wageni wengine.

Mdahala huo kwa jina ‘Mjadala Afrika’  unalenga kukuza dhamira ya tume ya umoja wa Afrika na kuwapa wagombea jukwaa la kuwakilisha maono yao ya kufikia lengo la shirika la Afrika lenye umoja, ustawi na amani.

Mdahalo huo utawasilishwa kwa lugha sita rasmi za muungano wa Afrika ikiwemo Kiingereza, Kifaransa, Kiarabu, Kireno, Kihispania na Kiswahili.

Mjadala huo utajikita katika masuala ya sera na ushiriki wenye mwelekeo wa suluhu kuhusu jinsi kila mgombea ananuia kuendeleza utimilifu wa matarajio na malengo ya agenda ya mwaka wa 2063.

Mjadala huu unaashiria wakati muhimu katika kampeni ya nafasi ya juu ya uongozi wa tume ya umoja wa Afrika. Hii itapatia wagombea nafasi ya kuonyesha uelewa wao wa changamoto za Afrika na kueleza jinsi watakavyo fanya ili kuzisuluhisha na kuliona bara la Afrika likiendelea.

Raila amefanya msururu wa  safari katika nchi kadhaa za Afrika akitafuta uungaaji mkono katika azma yake ya kuchaguliwa kama mwenye kiti wa tume ya umoja wa Afrika.

Ikiwa Raila atachaguliwa katika uchaguzi utakaofanyika February 2025 basi atakuwa Mwenyekiti wa kwanza kutoka Afrika Mashariki kuliongoza tume hicho. Vile vile atakuwa Mwenyekiti wa tano wa tume hicho baada ya Mwenyekiti anayeondoka Moussa Faki.

Raila atakuwa katika mdahalo huo pamoja na waziri wa mambo ya nje wa Djibouti Mahamoud Ali Youssouf na aliyekuwa waziri wa mambo ya nje wa Madagascar Richard Randriamandrato.

Hii ni baada ya  aliyekuwa waziri ya masuala ya nje wa Mauritius Kumarsingh Gayana kujiondoa katika kinyanganyiro hicho na kuunga mkono Raila Odinga.



RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved