KAMPUNI ya kusambaza umeme nchini Kenya (KPLC) imeonya kuhusu kukatizwa kwa umeme katika maeneo kadhaa nchini siku ya Jumatatu, Desemba 16.
Katika taarifa ya Jumapili jioni, kampuni hiyo ilisema kukatizwa kwa umeme kutatokana na ukarabati ambao utakuwa ukifanyika kwenye mitambo.
Walisema baadhi ya maeneo ya kaunti tatu za Kenya yatakosa umeme kati ya saa mbili asubuhi na saa kumi na nusu jioni. Kaunti ambazo zitaathirika ni Bomet, Embu, na Kisumu.
Katika kaunti ya Bomet, baadhi ya sehemu za eneo la Siongiroi zitaathirika na kukatizwa kwa umeme kati ya saa mbili asubuhi na saa kumi unusu jioni.
Sehemu za maeneo ya Embu University na Mountain Breeze katika kaunti ya Embu pia zitaathirika kati ya saa mbili unusu asubuhi na saa kumi unusu jioni.
Eneo la West Kano Irrigation Scheme katika kaunti ya Kisumu vilevile litaathirika kati ya saa tatu asubuhi na saa tisa alasiri.