KAMPUNI ya kusambaza umeme nchini Kenya (KPLC) imeonya kuhusu kukatizwa kwa umeme katika maeneo kadhaa nchini siku ya Jumanne, Desemba 17.
Katika taarifa ya Jumatatu jioni, kampuni hiyo ilisema kukatizwa kwa umeme kutatokana na ukarabati ambao utakuwa ukifanyika kwenye mitambo.
Walisema baadhi ya maeneo ya kaunti saba za Kenya yatakosa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.
Sehemu za maeneo ya Mulot, Sachora, na Baraka katika kaunti za Bomet na Narok zitakosa umeme kati ya saa mbili asubuhi na saa kumi unusu alasiri.
Maeneo ya Chepterit na Tulon katika kaunti ya Nandi yataathirika na kukatizwa kwa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.
Sehemu za eneo la Shinyalu katika kaunti ya Kakamega zitaathirika kati ya saa mbili asubuhi na saa kumi na moja jioni.
Maeneo ya Gogo na Sori katika kaunti ya Migori pia yataathirika kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi alasiri.
Katika kaunti ya Kirinyaga, sehemu za maeneo ya Kiarukungu, KHE, HCDA, Karurumo, na Kasafari zitakosa umeme kati ya saa mbili unusu asubuhi na saa kumi unusu alasiri.
Maeneo ya Slaughter Road na Cyton katika kaunti ya Kiambu pia yataathirika kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.