Katika taarifa iliyoandikwa na Royal house of the Netherlands ilisema kuwa ziara hiyo itaboresha uhusiano kati ya Kenya na Uholanzi na kuonyesha ushirikiano thabiti.
‘’Ziara hii ya kwanza ya kitaifa nchini Kenya ni uthibitisho wa uhusiano mzuri na ushirikiano thabiti kati ya nchi zetu mbili. Uholanzi inataka kushiriki katika ushirikiano mpya katika maeneo mbalimbali, na kuimarisha uhusiano uliopo wa nchi,’’ Hi ni kwa mujibu wa Royal House of Netherlands.
Katika ujumbe huo waliongezea kuwa Kenya inazidi kuwa na ushawishi mkubwa katika nyanja ya kimataifa huku Uholanzi na Kenya zikidumisha uhusiano wa karibu wa kiuchumi, na zote mbili ni vitovu na lango kuu kwa maeneo makubwa.
Ujumbe huo vile vile umeonyesha jinsi Uholanzi na Kenya zinaletwa pamoja na mashirika za kimataifa kama vile shirika la muungano la umoja la kitaifa maarufu kwa kimombo kama United Nations UN.
‘’Ndani ya umoja wa mataifa na mashirika mengine ya kimataifa, pia, nchi zetu mbili zinafanya kazi pamoja kikamilifu kufikia malengo yanayohusiana na demokrasia, utawala wa sheria na uhuru wa mahakama. Uholanzi na Kenya pia hufanya kazi pamoja katika changamoto zinazohusiana na amani na usalama, mabadiliko ya tabia nchi na usalama wa chakula,’’ Walisema haya katika ujumbe huo.
Majadiliano kuhusu uchumi inayoangazia kilimo endelevu na maji yatafanyika wakati wa ziara hiyo ya mfalme na malkia wa Uholanzi.
Ziara hii inakuja miaka miwili baada ya mfalme wa Uingereza Charles wa tatu na Malkia Camilla kufanya ziara sawa na hiyo nchini Kenya chini ya uongozi wa rais William Ruto. Wawili hao walitembelea Kenya kutoka tarehe 31 Octoba mapaka tarehe 3 Novemba 2023.