Rais William Ruto anatarajiwa kuanza ziara ya kina katika eneo la North Rift kuanzia Alhamisi 9, January 2025 hadi siku ya Jumamosi.
Kwenye ziara hiyo rais atazuri kaunti tatu katika eneo la North Rift ambapo ataanza na kutembelea kaunti ya Elgeyo Marakwet na kumalizia kwa Kaunti ya Uasin Gishu huku Transzoia Kaunti pia ikiwa miongoni mwa kaunti atakayozuru wakati huo wa ziara yake.
Wakati wa ziara hiyo rais Ruto anatarajiwa kuzindua miradi mbalimbali za maendeleo. Ruto ataangazia miradi ndani ya kaunti yake ya Uasin Gishu kwa siku mbili ambapo Gavana Jonathan Bii wa counti hiyo anasema wamefurahishwa na ziara ya Rais katika eneo hilo.
‘’Tuko tayari kumkaribisha Rais katika kaunti hii ya kifalme ili pamoja na wakazi wa Uasin Gishu tupate nafasi ya kujadili masuala ya maendeleo,” Alisema Bii katika ujumbe wake.
Baadaye Ruto atawasili Elgeyo Marakwet siku ya Alhamisi kwa ziara ya miradi ikijumuisha taasisi ya mafunzo ya kiufundi ya Kerio Valley, taasisi ya mafunzo ya matibabu ya Kerio Valley , taasisi ya mafunzo ya kiufundi ya Kapcherop pamoja na uzinduzi wa barabara ya Kapkundul-Kapyego-Kamelei huku akitarajiwa kutoa hatimiliki ya ardhi kwa wakazi hao.
Siku ya Ijumaa Ruto ataanza ziara ya kina Kaunti ya Uasin Gishu kwa kuzuru eneo bunge ya Kapseret ambapo atafungua bwawa la Kimuri na taasisi ya mafunzo ya kiufundi Ngeria. Baadaye siku hiyo ataelekea atazindua miradi mingine katika eneo bunge la Kesses ikiwemo bwawa la Karita na kisha mradi wa kuunganisha umeme wa Chebor maili ya mwisho.
Wakati wa ziara hiyo rais Ruto anatarajiwa kuzungumza na wakazi wa kaunti hizo hasa atakapokuwa anasafiri katika eneo hizo.
Ziara hii ya rais katika eneo la North Rift linakuja baada ya baadhi ya watu kulalamika kuwa amekuwa akifanya ziara mingi eneo la Nyanza tangia kuundwa kwa serikali yenye msingi mpana iliona wanachama wa chama cha ODM.