Moto mkubwa ulizuka katika ukumbi wa Taifa Hall katika chuo kikuu cha Nairobi Jumatano 15, Januari 2025 usiku, na kusababisha uharibifu mkubwa kwa jengo hilo.
Moto huo unasemekana kuanza katika jiko la mkahawa mmoja inayopakana na jengo hilo kabla ya kusambaa katika maeneo mengine. Jumba hilo vilevile inamiliki baadhi ya ofisi za chuo hicho.
Afisa mkuu wa kitengo cha polisi (OCPD) Stephen Okal alisema kuwa moto huo ulidhibitiwa usiku lakini ulizuka tena alfajiri.
Aliongezea kuwa moto mpya uligunduliwa na mmoja wa mlinzi wa chuo hicho Alhamisi asubuhi ya saa kumi na moja.
"Kikosi cha zima moto kilirudishwa kwenye eneo la tukio kusaidia kudhibiti moto huo. Wameweza kuidhibiti. Huu ni muundo wa kihistoria na uharibifu uliosababishwa ni mkubwa na tunatarajia kupata sababu ya moto huo,’’ Alisema afisa huyo.
Okal alisema kuwa wataalam watafanya uchunguzi kuhusiana na moto huo na hatua mwafaka kuchukuliwa .
Katika video iliyosambaa katika mitandao ya kijamii ilionyesha ukubwa wa moto huo, huku moshi na miali zikionekana chuoni kote.
Wakati wa mkasa huo wa moto ilibidi maafisa wa polisi kuitwa kusaidia kuwazuia watu waliokuwa na nia ya kuporar ambao walikimbilia eneo la tukio ili kutumia fursa hiyo kupora hata wakati timu ya watu kutoka zima moto wakipambana na kudhiti moto huo kuenea.
Mkasa huo wa moto unakuja wakati chuo hicho kiliratibu kuanzisha mitihani iliyocheleweshwa kutokana na mgomo wa waadhiri wa vyuo vikuu vya umma nchini mwaka jana. Tukio iliyolemaza shuguli za masomo chuoni.
Chuo kikuu cha Nairobi ndio kongwe zaidi nchini ikiwa kwamba ilianzishwa mnamo 1, Julai 1970. Ikiwa na miaka 55 tangia kuanzishwa rasmi kama chuo kikuu nchini.
Moto huo unazuka wakati chuo hicho inakabiliwa na changamoto wa usimamizi.