Aliyekuwa rais wa nne wa Jamhuri ya Kenya kati ya mwaka 2013 – 2022 Uhuru Muigai Kenyatta amewapongeza vijana wa Gen –Z wanavyojitokokeza na kuendelea kupigania haki yao.
Kenyatta amewapa kongole vijana wa Gen-Z akiwahimiza kuendelea kupigania haki yao kwani wao ndio tegemeo la baadaye na kizazi cha kesho.
“Shida ya watu siku hizi ni kuogopa, MaGen – Z nyinyi ndio tegemeo la baadaye, piganieni haki zenu sio kukaa tu mkiacha mali yenu ichukulie na mmeitolea jasho, pambaneni mhakikishe mnachukua haki yenu,” alisema rais msitaafu Uhuru Kenyatta .
“Kila kitu lazima mkipiganie , msipopigania kitaenda mali yenu itachukuliwa na mtu asilie. Wale walitekwa si waltokaka na kuendelea na maisha na tuko nyuma yenu”.
Rais mstaafu alizungumza haya huku pia akimshawishi bintiye kujiunga na Gen- Z kuliko kendelea kuwa mpole zaidi.
Haya yanakuja
muda mchache tu baada ya Uhuru Kenyatta kukutana na rais William Ruto mwezi na
baadhi ya mawaziri waliokuwa katika serkali ya Kenyatta kuteuliwa na Rais Ruto
na kujiunga na serikali