Gavana wa Nairobi Johnson Sakaja ametangaza makataa mapya ya siku 90 kwa wamiliki wa nyumba katikati mwa jiji kuyapaka rangi upya.
Sakaja akitoa masharti hayo amewataka wamiliki kurekebisha majumba yao, kuyapaka rangi upya pamoja na kuweka mwangaza wa kusaidia walinzi hasa nyakati za usiku.
" Kama njia moja ya kutia bidii katika kuhakikisha usafi na kuinua kiwango cha jiji letu kuu, wamiliki wa majumbaa katikati mwa jijia watatakiwa kurejelea kupaka upya rangi majumba yao na kuweka mwangaza panapiostahili. Chapisho kuhusu hili litatolewa wiki hii na na tutawapea siku 90 kukamilisha takwa hilo."
Johnson Sakaja amsema hili baada kuonekana kuongoza katika shughuli za kusafisha mji siku chache zilizopita hasa nyakati za usiku.
Baadhi ya shughuli zilizofanywa katikati mwa jiji ni pamoja na chati za matangazo ya biashara ambazo hazijalipiwa ushuru, pamoja na biashara zisizo chini ya sheria.
Johnson Sakaja ni Gavana wa nne kuliongoza jiji la Nairobi, alichukua usukani mwaka 2022 kutoka kwa Ann Kananu Mwenda baada ya kutua ushindi katika uchaguzi wa kitaifa uliofanyika 2022 na kumpiku mshindani wake wa karibu Polycarp Igathe.
Baadhi ya magavana ambao wamewahi kuliongoza jiji la Nairobi ni pamoja na aliyekuwa Gavana wa kwanza Evans Kidero kati ya mwaka wa 2013-2017. Mike Mbuvi Sonko kati ya mwaka 2017 -2020, Sonko Alibanduliwa mamulakani kabla ya kumaliza muhula wake wa kwanza ambao ni miaka mitano kulingana na katiba ya kenya.