Waziri mkuu katika serikali ya kenya kwanza Musalia Mudavadi amemuonya aliyekua naibu wa rais Rigathi Gachagua kujitenga na siasa.
Mudavadi alikuwa akihutubia wananchi katika kaunti ya Kakamega Jumanne 21 katika safari ya rais William Ruto kutua magharibi kwa ajili mipango ya kuinua taifa huku akielekeza maneno yake kwa aliyekuwa naibu wa rais Rigathi Gachagua.
Alisema kuwa ni wakati wa kenya kuunganishwa na kusonga mbele, bali sio ukabila wala wakati wa mtu kulia kuwa aliondolewa mamlakani uliisha ashughulike na mambo mengine.
"Kama mtu alikua analia, wakati huo umeisha, Kenya lazima isonge mbele, nchi haiko hapo kukusikiza ukilia kila siku.Hatutaki mambo ya ukabila Kenya lazima isonge mbele na hivyo ndivyo rais Ruto anafanya," alisema Mudavadi.
Kwa kile kilichoonekana kama kufafanua sheria ya katiba ya kenya ailimuonya Gachagua kwamba hawezishikia nafasi yoyote katika ofisi ya umma na ingekua vyema asonge mbele na kujishughulisha mambo mengine kuliko kuendelea kupiga kelele za kuwapotosha wananchi.
"Sheria inasema hivi, kama wewe umebanduliwa mamlakani, hauwezi kushikilia nafasi yoyote katika ofisi ya umma, hata nyumba kumi hutapata,"
Mudavadi amewataka wananchi kuchukua sheria, kuisoma na kuilewa vilivyo kuliko kuharibu muda kupotoshwa na mtu ambaye haezishikilia wadhifa katika ofisi ya umma. Alieleza kwamba sheria inaeleza vizuri kuhusu mtu aliyebanduliwa mamlakani.
waziri huyo mkuu akilinganisha tukio hili la na matukio ya magavana wailondolewa mamlakani, aliekuwa governor wa kaunti ya Nairobi Mike Sonko na aliyekuwa governor wa kaunti ya Kiambu Fednand Waititu ambao mpaka sasa hawajawania nafasi yoyote ya kisiasa au kushikilia wadhifa wowote wa ofisi ya uma katika taifa la Kenya tangu walipong'olewa mamlakani.
Sonko na Waititu wote waliondolewa mamlakani na wawakilishi wadi kutokana na utovu wa nidhamu katika ofisi zao na kuidhinishwa na bunge la seneti kulingana na katiba ya kenya.