KAMPUNI ya kusambaza umeme nchini Kenya (KPLC) imeonya kuhusu kukatizwa kwa umeme katika maeneo kadhaa nchini siku ya Jumanne, Januari 21.
Katika taarifa ya Jumatatu jioni, kampuni hiyo ilisema kukatizwa kwa umeme kutatokana na ukarabati ambao utakuwa ukifanyika kwenye mitambo.
Walisema baadhi ya maeneo ya kaunti kumi za Kenya yatakosa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.
Kaunti ambazo zitaathirika ni pamoja na Nairobi, Nakuru, Nandi, Uasin Gishu, Kisumu, Bungoma, Nyeri, Laikipia, Kiambu, na Mombasa.
Katika kaunti ya Nairobi, sehemu za eneo la Kahawa West zitakosa umeme kati ya saa tisa asubuhi na saa kumi na moja jioni.
Sehemu za maeneo ya Milimani, PGH, na Forest Rd katika kaunti ya Nakuru zitaathirika kati ya saa tatu asubuhi na saa tisa alasiri.
Maeneo ya Lolduga, Lessos Junction, na Mogobich katika kaunti ya Nandi yataathirika kati ya saa mbili asubuhi na saa kumi na moja unusu jioni.
Katika kaunti ya Uasin Gishu, maeneo ya Kitingia, Kondoo Cheberer, Burnt Forest na Ainabkoi yataathirika kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.
Eneo la Soko ya Chemelil katika kaunti ya Kisumu litaathirika na kukatizwa kwa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi alasiri.
Maeneo ya Karogoto, Thamaru, Gatitu, na Kiawaithanji katika kaunti ya Nyeri yataathirika kati ya saa mbili asubuhi na saa kumi na moja jioni.
Sehemu za Nturukuma na Kangaita katika kaunti ya Laikipia pia yataathirika kati ya saa mbili unusu asubuhi na saa kumi alasiri.
Katika kaunti ya Kiambu, maeneo ya Ndura, Fourteens Falls na Kolping yataathirika kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.
Sehemu za maeneo ya Vitengeni, Bamba Ganze, na Matano Manne katika kaunti ya Mombasa yatakosa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.