Rais william Ruto amefadhaika na maneno ya Kalonzo kuongoza Maandamano.
Kiongozi wa chama cha Wiper Kalonzo Musioka alitishia kuongoza maandamano kushurutisha serikali kubuni tume ya uchaguzi ya IEBC, kuanzia mwezi wa tatu iwapo tume haitakuwa imebuniwa.
Rais Ruto ameonesha kuwajibu moja kwa moja watu wa upinzani walipodai kwamba serikali imetumia pesa ya wananchi kuwapa bonas wakulima wa miwa wa kampuni ya Mumias.
Upinzani umetaja hilo kuwa lisilofaa na Rais anatumia pesa ya wananchi kutafuta uungwaji mkono magharibi.
Rais amewajibu akisema waache uwoga na huo ni msururu wa maendeleo tu wala kampeni haijaanza.
"Acheni uwoga wa mapema, siasa bado, mnasema hii sasa, tukianza siasa yenyewe si mtakimbia. hii ni mambo ya maendele kwanza," rais alisema.
Ruto akionekana kuwajibu watu waliokuwa wakiuliza ni vipi serikali iliwapa wakulima bonus wakati kampuni ya Mumia inaandamwa na madeni chungu nzima.
"wanauliza mbona serikali imesaidia watu wa Mumias mpaka imelipa bonus wakulima wa miwa, kwani mkulima wa miwa si mkenya, kama vile wakulima wa kahawa na majani wanavyolipwa bonas, ndivyo wakulima wa miwa pia wanafaa kushugulikiwa.
Hayo maswali ya hawa watu ni kama wameingiliwa na shetani. mahali bonus ya kulipa wakulima wengine hutoka ndo tulitoa pesa ya kulipa wakulima wa miwa. tutafanya hivyo kwa kampuni zote za miwa," rais Ruto alieleza.
Rais alikua anazungumza katika kaunti ya Busia kwenye ziara yake ya kuzuru maeneo ya magharibu.