logo

NOW ON AIR

Listen in Live

NYS yatangaza nafasi za kazi 387 nchini Israel

Waombaji kazi watakaofaulu watalipwa kati ya Sh250,000 na Sh350,000 kwa mwezi.

image
na Samuel Mainajournalist

Yanayojiri24 January 2025 - 16:01

Muhtasari


  • Katika notisi hiyo iliyotolewa Ijumaa, wahitimu wa NYS wanaovutiwa na nafasi za kazi 387 zinazopatika wamesihiwa kutuma maombi.
  • Watatakiwa kufanya kazi hadi saa sita kwa siku nzima na hadi saa nane kwa nusu siku.


Huduma ya Kitaifa ya Vijana (NYS)  imetangaza fursa za kazi nchini Israeli kwa wahitimu wake.

Katika notisi hiyo iliyotolewa Ijumaa, wahitimu wa NYS wanaovutiwa na nafasi za kazi 387 zinazopatika wamesihiwa kutuma maombi.

Nafasi hizo ni pamoja na nafasi 80 za maseremala wa ujenzi, 80 za warekebishaji chuma, 50 za wapiga plasta, 40 za wahudumu wa mashine nzito, 30 za mafundi bomba na 20 za mafundi umeme.

Pia kuna nafasi 50 za waashi vigae, nafasi 10 za uhandisi, nane za msimamizi -useremala, nane za usimamizi wa ufundi wa chuma, sita za usimamizi wa plaster na tano za usimamizi wa uashi.

Waombaji watakaofaulu watalipwa kati ya Sh250,000 na Sh350,000 kwa mwezi.

Gharama ya usafiri, Visa, gharama ya mafunzo kabla ya kuondoka na gharama ya uchunguzi wa kimatibabu itagharamiwa na mwombaji kazi.

"Huu utakuwa mchakato unaoendelea huku kundi la kwanza likitarajiwa kuanza shughuli hiyo kuanzia Jumanne, Januari 28, 2025," Mwakilishi Mkuu Samson Kiptum alisema kwa niaba ya Kamanda Mkuu.

Kiptum alisema watahiniwa wanaokidhi mahitaji ya kazi watawasiliana nao kwa ajili ya majaribio ya vitendo (mahojiano) katika Taasisi ya Kitaifa ya Uhandisi wa Huduma ya Vijana kwa vikundi kuanzia Januari 28, 2025.

Kulingana na notisi, wafanyikazi wa ujenzi waliofaulu watahitajika kufanya kazi kwa muda wa miezi 63 ( sawa na miaka mitano na miezi mitatu).

Watatakiwa kufanya kazi angalau saa 236 (katika mwezi kamili wa kazi) siku sita kwa wiki Jumapili hadi Ijumaa (Jumapili hadi Alhamisi ni siku kamili, Ijumaa ni nusu siku), Jumamosi ni siku ya kupumzika.

Watatakiwa kufanya kazi hadi saa sita kwa siku nzima na hadi saa nane kwa nusu siku.

Mshahara wa kimsingi kwa saa utakuwa Shekeli Mpya za Israeli 32.30, takriban Sh1,116.

Pia watakuwa na haki ya saa za ziada, nyumba zinazotolewa na kampuni, na makato ya kila mwezi kulingana na sheria za kazi za Israeli.

Usafiri, vifaa vya kibinafsi na vya kazi na mafunzo ya urefu na usalama yatatolewa na mwajiri, wakati likizo ya ugonjwa itakuwa kulingana na sheria ya kazi ya Israeli.

Wale wanaovutiwa na nafasi hizo wameshauriwa kupitia sifa na maelezo ya kazi kama ilivyoainishwa na NYS.

https://docs.google.com/document/d/1bEj8ypFdZwlkRWIWCU2Yg_J8x9rpejENh3zyYgkRLGI/edit?tab=t.0

Waombaji wanaokidhi mahitaji wameelekezwa kutuma maombi kwa kufungua na kujaza fomu katika link: https://forms.gle/vdbCQEvF5Xq6dNmw7



RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved