Serikali ya kenya imetangaza kuhamisha mpango wa pesa zote za inua jamii kufikia wananchi kupitia njia ya M Pesa.
Katibu mkuu wa wizara husika Joseph Motari hapo jana Januari 23 alisema kwamba watu wote wanaonufaika na programu ya Inua Jamii watapokea mgao wao kupitia njia ya simu.
Ameeleza kwamba hilo litaanza kutendeka kuanzia Januari hii na watazipata pesa hizo kupitia kubonyeza *222 kutumia laini ya kampuni ya Safaricom.
"Watu wote wanaonufaika na Inua Jamii watatakiwa kuhakikisha laini yao ya m pesa imesajiliwa vilivyo kwa majina yao ili wapate pesa zao," alisema Motari.
Motari aliongeza kwamba wale ambao wana laini za safaricom wanafaa kuhakikisha ziko sawa na wale hawana wajisaji.
Amewataka wale ambao watashindwa wafike katika office ili kupata usaidi au wapige simu kupitia 1533, bila malipo ya hudhuma.
Baadhi ya ofisi ni kama; County/ Sub - county Social Development office, Sub-County Childrens Office, county Disability Offices.
Programu ya Inua Jamii sasa inawasaidia zaidi ya watu milioni1.7, wakiwemo watoto kutoka katika familia zisizojiweza, watoto yatima, watu wenye mapungufu pamoja na watu wenye miaka 70 na kuendelea kutoka katika familia masikini.
Pesa hizo huja kila mwezi ili kuwasaidia kupigana na lindi la umasikini na makali ya njaa.
Rais Wiliam Ruto akizungumzia hili siku chache zilizopita alisema kwamba fedha hizo kutumwa kupitia njia ya simu itasaidia pakubwa.Alisema kwamba imekuwa ikiwagharimu wahusika kusafiri kwa mwendo mrefu ili kufika kwenye benk kila mwezi jambo ambalo ni changamoto kubwa hasa kwa watu wenye umuri mkubwa.
Kulingana na takwimu za mwezi jana Serikali ilitoa bilioni 3.5 ili kuwawafikia watu watu milioni 1.5 kila mmoja akipata shilingi elfu mbili.