logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Gachagua afanya mazungumzo na Martha Karua nyumbani kwake Kirinyaga

Gachagua aliwasili katika nyumbani kwa Karua Jumamosi mchana akiandamana na mkewe Dorcas Rigathi.

image
na JAMES MBAKAjournalist

Yanayojiri25 January 2025 - 14:51

Muhtasari


  • Huu ni mkutano mkuu wa kwanza wa kisiasa ambao Gachagua anafanya na Karua tangu kuondolewa madarakani kama naibu rais.
  • Mkutano huo huenda ukaibua mijadala ya kisiasa kuendelea huku Gachagua akijaribu kuunganisha eneo la Mlima Kenya.


Kiongozi wa chama cha Narc-K Martha Karua na naibu rais aliyetimuliwa Rigathi Gachagua wamefanya mkutano wa mashauriano siku ya Jumamosi.

DP huyo wa zamani aliwasili katika nyumbani kwa Karua Jumamosi mchana akiandamana na mkewe Mchungaji Dorcus Rigathi.

Mazungumzo hayo  yalijiri saa chache baada ya Msajili wa Vyama vya Kisiasa kutangaza kwenye gazeti la serikali kwamba UDA inakusudia kumuondoa aliyekuwa Naibu Rais Rigathi Gachagua kama naibu kiongozi wa chama.

Katika notisi ya gazeti la serikali ya Januari 23, Anne Nderitu aliarifiwa kuhusu nia ya UDA kubadilisha nafasi ya Gachagua na kumpa naibu wa Rais Kithure Kindiki.

“Mtu yeyote mwenye maoni ya maandishi kuhusu mabadiliko yaliyokusudiwa na chama cha siasa ndani ya siku saba (7) kuanzia tarehe ya chapisho hili, atatoa maoni yake kwa maandishi kwa Msajili wa Vyama vya Siasa,’’ inasomeka notisi hiyo.

Huu ni mkutano mkuu wa kwanza wa kisiasa ambao Gachagua anafanya na Karua tangu kuondolewa madarakani kama wa kiongozi wa pili nchini Kenya.

Mkutano huo huenda ukachagiza mijadala ya kisiasa kuendelea huku Gachagua akijaribu kuunganisha eneo la Mlima Kenya.

Karua alikuwa mkosoaji mkuu wa Gachagua kabla ya uchaguzi mkuu wa 2022 akiwa mgombea mwenza wa waziri mkuu Raila Odinga.

Pia aliibuka kama mkosoaji mkubwa wa serikali ya Kenya Kwanza baada ya kura za 2022 na wakati wa maandamano dhidi ya serikali ambayo yalitikisa nchi.

Mkutano huo pia unajiri wakati ambapo Narc Kenya ya Karua inafanya mabadiliko baada ya kujiondoa katika muungano wa Azimio.

Mapema Januari, Karua alianzisha mchakato wa kisheria wa kubadilisha jina la Narc Kenya kuwa People’s Liberation Party (PLP).

Hatua ya hivi punde zaidi inapelekea vita vya wapiga kura wa Gen Z nchini humu kuwa juu zaidi huku idadi ya watu ikitarajiwa kuunda idadi kubwa ya wapiga kura 2027 nchini Kenya.

Takwimu za Baraza la Kitaifa la Idadi ya Watu na Maendeleo la Kenya zilionyesha katika sensa ya 2019 kuwa asilimia 75.1 ya watu wa Kenya walikuwa chini ya umri wa miaka 35.

Hata hivyo inaarifiwa kuwa Gachagua anatazamiwa kuzindua chama chake mapema mwezi Februari huku akiweka msingi wa uchaguzi mkuu wa 2027.

Washirika wa zamani wa DP wamethibitisha kuwa mipango ya kuzindua gari la kisiasa imekamilika huku Gachagua akijaribu kudhibitisha ushawishi wake katika siasa za kitaifa.

Pia anataka kuunganisha kitovu chake cha Mlima Kenya, ambacho kimekuwa kikipinga serikali tangu kuondolewa kwake afisini.

Haijulikani ikiwa DP wa zamani atapata chama kilichopo au kuzindua chama kipya cha kisiasa kilichosajiliwa.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved