KAMPUNI ya kusambaza umeme nchini Kenya (KPLC) imeonya kuhusu kukatizwa kwa umeme katika maeneo kadhaa nchini siku ya Jumanne, Januari 28.
Katika taarifa ya Jumatatu jioni, kampuni hiyo ilisema kukatizwa kwa umeme kutatokana na ukarabati ambao utakuwa ukifanyika kwenye mitambo.
Walisema baadhi ya maeneo ya kaunti tatu za Kenya yatakosa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.
Kaunti ambazo zitaathirika ni pamoja na Nairobi, Nyeri, na Embu.
Katika kaunti ya Nairobi, baadhi ya sehemu za maeneo ya Ruaraka, Kibera, Lang'ata na Karen zitaathirika na kukatizwa kwa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.
Maeneo ya Sagana State Lounge, soko ya Iruri, Muthinga, na Kangubiri katika kaunti ya Nyeri yataathirika kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.
Maeneo ya Embu College, Kanjuru Estate, Kenstar Hardware, Irangi Food Processing na sehemu za soko ya Shauri katika kaunti ya Embu pia yataathirika kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi alasiri.