Hakimu Mohammed Noor Kullow Jumatatu Februari 3 ,2025 amepata afueni baada ya kamati iliyoundwa na rais kumpiga msasa kwa kuchunguza madai yaliyoibuiwa dhidi yake kumpata bila hatia.
Jaji Noor Kullow alikuwa amesimamishwa kazi na rais William Ruto mnamo Machi 2024 kufuatia pendekezo kutoka kwa kamati ya kuchunguza mienendo ya majaji nchini( JSC) iliyoibua madai kuwa Jaji Noor alikuwa na mienendo mibaya, alikiuka katiba na alivunja kipenge cha tume ya mienendo ya majaji kuhusu maadili ambacho kilinakiliwa mwaka 2020 miongoni mwa makosa mengine.
Baada ya uchunguzi uliodumu kwa takribani miezi mitano, mwenyekiti wa kamati ya uchunguzi jaji Patrick Kiage wa mahakama ya rufaa aliwasilisha ripoti kwa rais iliyompata jaji Noor bila kosa lolote lililoibuliwa dhidi yake.
Katika ripoti iliyowasilishwa kwa rais na mwenyekiti jaji Kiage alimrai rais kumteua upya tena kuwa jaji na kumteua kuwa jaji wa mazingira na ardhi.'
"Mheshimiwa rais baada ya kuangazia ushahidi uliowasilishwa mbele ya kamati ya kupiga msasa makosa ya jaji Mohammed Noor, dai la kwanza, pili, tatu, nne, tano, sita, saba, nane, tisa, kumi, kumi na moja, kumi na mbili na kumi na tatu hayajaafikia viwango vinavyohitajika kumtimua tumebaini kuwa jaji Noor hakuvunja kipengee chochote cha maadili kipengee nambari 168 1 (b) na (e) vya katiba maelezo ya ripoti yalisema.
''Kulingana na mujibu wa kifungu nambari 168(7) cha katiba, kwa hivyo tunapendekeza umteue upya jaji Mohamed Noor Kullo kama jaji wa mazigira na ardhi''
Shitaka jingine ambalo lilikuwa limewasilishwa dhidi ya jaji Noor ni alikuwa amekawia kutoa hukumu katika maamuzi mbalimbali ya kesi za awali mshitaki akisisitiza kuwa alionyesha kutowajibika ipasavyo ijapokuwa kamati ya uchunguzi iliafikia uamauzi kuwa kutotoa uamuzi kwa wakati haikumanisha kuwa hakuwa na uwezo wa kutoa maamuzi ikizingatiwa kuwa hapo awali alikuwa akitoa uamuzi wake ipasavyo.
Katika shitaka jingine jaji alishitakiwa kwa kosa la kutoa uamuzi wa kukanganya, kamati ikipiga msasa na kubaini kuwa shitaka hilo lilikosa ushahidi wa kutosha hivyo ikatupilia mbali kwa kuzingatia hayo yote na kupiga msasa madai yote yaliyoibuliwa na wakosoaji wake kamati ilibaini na kuafikia uamuzi kuwa kwa makosa yote yaliyosemwa hamna kosa lolote lililoafikia viwango vya jaji Noor kusimamishwa kazi au kutimuliwa badala yake kamati ilimpendekezea rais ampe jaji Noor majumu mengine ya kazi aendelee kuchapa kazi.