logo

NOW ON AIR

Listen in Live

DCI yathibitisha kurejesha udhibiti wa akaunti za X na Faceebook baada ya kudukuliwa

DCI imetangaza kwamba imefaulu kurejesha umiliki wa mitandao yake ya kijamii.

image
na Japheth Nyongesa

Yanayojiri10 February 2025 - 10:07

Muhtasari


  • Kwa muda huo mchache wahalifu wa mitandao walichapisha maandishi yasiyo ya kweli na kwa hivyo DCI imeyataja kama yasiyo ya kweli.
  • Shambulio hilo katika ukurasa wa DCI ni la hivi punde miongoni mwa mengine mengi ambayo yamegonga akaunti za mitandao ya kijamii katika wiki chache zilizopita.

DiRECTO

DCI imetangaza kwamba imefaulu kurejesha umiliki wa mitandao yake ya kijamii.

Mitandao ya X  na Facebook ya DCI ilikuwa imedukuliwa na wahalifu wa mitandao kwa masaa kadhaa.

Jumapili ya tarehe tisa 2025 DCI ilitoa tangazo na kukubali kwamba akaunti zake zillikuwa zimetekwa na wahalifu wa mitandao ila wakawahakikishia Wakenya kwamba umiliki wote ulikua umerejeshwa na kila kitu kilikuwa sawa.

"Kwa muda mfupi jioni hii tulipata shambulio la kimtandao kwenye majukwaa ya kidijitali X na Facebook ya DCI lakini tangu wakati huo tumepata udhibiti kamili" DCI ilisema.

Kwa muda huo mchache wahalifu wa mitandao walichapisha maandishi tatanishi na kwa hivyo DCI imeyataja kama yasiyo ya kweli.

"Kwa muda huo mchache ambao wahalifu wa mitandao walikuwa wanajaribu kuchukua mitanandao  wamechapisha habari za kupotosha," DCI ilikiri.

"Mahojiano katika shughuli za uhalifu yameanzishwa ili kuleta kwenye kitabu wahusika,"  DCI ilisisitiza.

Shambulio hilo katika ukurasa wa DCI ni la hivi punde miongoni mwa mengine mengi ambayo yamegonga akaunti za mitandao ya kijamii katika wiki chache zilizopita.

Wakenya walishtuka baada ya taarifa zinazohusiana na utapeli wa sarafu ya kidijitali na ulaghai wa blockchain kuwekwa kwenye kurasa hizo siku ya Jumapili, na kutuma ishara za wazi kwamba walikuwa chini ya udhibiti wa wadukuzi.

Kisa hicho cha udukuzi kinakuja wiki moja tu baada ya Kituo cha Utangazaji cha Kenya (KBC) kufichua kuwa ni mwathirika wa shambulio la kimtandao.

Shambulio jingine lilikabili K24 TV ambayo ilidukuliwa wiki iliyopita na kuona ukurasa huo ukibadilishwa jina mara kadhaa.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved