logo

NOW ON AIR

Listen in Live

KPLC Yatangaza Kaunti 11 Zitakazoathirika Na Kukatizwa Kwa Umeme Leo, Jumanne

KPLC imeonya kuhusu kukatizwa kwa umeme katika maeneo kadhaa nchini siku ya Jumanne, Februari 11.

image
na Samuel Mainajournalist

Yanayojiri11 February 2025 - 07:14

Muhtasari


  • Kampuni ya KPLC imesema kukatizwa kwa umeme kutatokana na ukarabati ambao utakuwa ukifanyika kwenye mitambo.
  • Wamesema baadhi ya maeneo ya kaunti 11 za Kenya yatakosa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.

caption

KAMPUNI ya kusambaza umeme nchini Kenya (KPLC) imeonya kuhusu kukatizwa kwa umeme katika maeneo kadhaa nchini siku ya Jumanne, Februari 11.

Katika taarifa ya Jumatatu jioni, kampuni hiyo ilisema kukatizwa kwa umeme kutatokana na ukarabati ambao utakuwa ukifanyika kwenye mitambo.

Walisema baadhi ya maeneo ya kaunti 11 za Kenya yatakosa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.

Kaunti ambazo zitaathirika ni pamoja na Nairobi, Kisumu, Siaya, Vihiga, Homa Bay, Tharaka Nithi, Nyeri, Meru, Embu, Laikipia, na Mombasa.

Katika kaunti ya Nairobi, sehemu za maeneo ya Kasarani na Githurai 44 zitaathirika na kukatizwa kwa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.

Soko ya Holo katika kaunti ya Kisumu pia itaathirika na kukatizwa kwa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.

Mitaa ya South Lands na Randogo katika kaunti ya Siaya itaathirika kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.

Soko ya Majengo katika kaunti ya Vihiga itakosa umeme kati ya saa mbili unusu asubuhi na saa kumi na moja jioni.

Sehemu za maeneo ya Rambusi na Kodiera katika kaunti ya Homa Bay zitaathirika kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi alasiri.

Maeneo ya Kaare na Muragara katika kaunti ya Tharaka Nithi yataathirika kati ya saa mbili unusu asubuhi na saa kumi alasiri.

Maeneo ya Kianjogu Coffee factory, Munyu, Kimahuri, na mji wa Narumoro katika kaunti ya Nyeri yataathirika kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.

Eneo la Tulivu Gardens katika kaunti ya Meru litaathirika kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.

Katika kaunti ya Laikipia, maeneo ya Makutano na Embori yataathirika kati ya saa mbili asubuhi na saa kumi alasiri.

Maeneo ya Kilifi Corner Makadara, Changamwe, na Miritini katika kaunti ya Mombasa pia yataathirika kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.



RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved