KAMPUNI ya kusambaza umeme nchini Kenya (KPLC) imeonya kuhusu kukatizwa kwa umeme katika maeneo kadhaa nchini siku ya Alhamisi, Februari 13, 2025.
Katika taarifa ya siku ya Jumanne jioni, kampuni hiyo ilitangaza kwamba baadhi ya maeneo ya kaunti 11 za Kenya yatakosa umeme kati ya saa mbili asubuhi na saa kumi na moja jioni.
Kaunti ambazo zitaathirika na kukatizwa kwa umeme ni pamoja na Nairobi, West Pokot, Vihiga, Tharaka Nithi, Nyeri, Embu, Laikipia, Kiambu, Kitui, Kwale, na Tana River.
Katika kaunti ya Nairobi, sehemu za maeneo ya Mukuru Kwa Njenga na Pipeline zitakosa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.
Eneo la Alale katika kaunti ya West Pokot litaathirika na kukatizwa kwa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa tisa alasiri.
Eneo la shule ya Vihiga Boys litakosa umeme kati ya saa mbili unusu asubuhi na saa kumi na moja jioni.
Maeneo ya Ciakariga, na Marimanti Prison katika kaunti ya Tharaka Nithi pia yataathirika kati ya saa mbili unusu asubuhi na saa kumi unusu alasiri.
Sehemu za maeneo ya Kiganjo na Ndurutu katika kaunti ya Nyeri zitakosa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.
Maeoneo ya Kyeni Girls, Nthokis Hotel, na Mugoya Police katika kaunti ya Embu yataathirika na kukatizwa kwa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.
Katika kaunti ya Laikipia, maneo ya Bantu Lodge, Gathiuru na Mureru yataathirika kati ya saa mbili asubuhi na saa kumi alasiri.
Maeneo ya Pascha na Wangware katika kaunti ya Kiambu yataathirika kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.
Maeneo ya Ngiini na Mutune katika kaunti ya Kitui yataathirika kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.
Maeneo ya Tsunza na Mwache katika kaunti ya Kwale yataathirika kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.
Sehemu za maeneo ya Hola, Bura na Masalani katika kaunti ya Tana River pia zitakosa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa saba mchana.