KAMPUNI ya kusambaza umeme nchini Kenya (KPLC) imeonya kuhusu kukatizwa kwa umeme katika maeneo kadhaa nchini siku ya Jumapili, Februari 16.
Kaunti ambazo zitaathirika ni Nairobi, Uasin Gishu, Kiambu, na Kilifi.
Katika kaunti ya Nairobi, sehemu za mtaa wa Kileleshwa zitaathirika na kukatizwa kwa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.
Sehemu za maeneo ya Jua Kali, na Simba Cement katika kaunti ya Uasin Gishu zitakosa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi alasiri.
Baadhi ya sehemu za maeneo ya Kihunguru, Rainbow na NKG katika kaunti ya Kiambu pia zitakosa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.
Wakati huohuo, sehemu za maeneo ya Malindi Complex, Malindi Police, na Golf pia zitaathirika na kukatizwa kwa umeme.