Mshukiwa aliyemteka nyara Mtoto Kiambu
Mwanamme wa miaka 33 kwa jina Joseph Murith Kibutu alikamatwa na makachezo wa DCI kwa madai ya kumteka nyara mvulana wa miaka saba mtaa wa Mwihoko kaunti ya Kiambu mnamo Februari 17,2025.
Hii ilitokana na ushirikiano wa hali ya juu kati ya maafisa wa polisi wa kituo cha Githurai na maafisa wa DCI.
Jambo hili liligundulika wakati ambapo wazazi wa mtoto huyo
walipogundua kuwa mwanawe hayupo walipokuwa wakinunua bidhaa katika duka kuu la
Savory mtaa wa Mwihoko.Ghafla walitanabahi kupata mwanao hayupo licha ya juhudi
za kumtafuta kugonga mwamba.
akiwa katika hali ya kuchanganyikiwa walipigiwa simu kutoka kwa mtu wasiye mfahamu aliyesema kuwa yeye ndiye aliyekuwa na mwanao na kuitisha kitita cha shilingi elfu mia moja(100,000) akiwahakikishia kuwa angemrejesha mwana kwa masharti ya kulipwa mwanzo.
Maafisa wa polisi walilichukulia suala hilo kwa uzito na kuanzisha uchunguzi wa haraka ili kumtafuta mhusika huyo na kumtoa mafichoni,kutokana na upelelezi wa hali ya juu mhusika huyo aliweza kunaswa akiwa mafichoni maeneo ya Githurai mtaa wa Reli.
Hatimaye walifanikiwa kumkamata mhusika Pamoja na mtoto ambaye alikuwa amefichwa na kumpokeza kwa wazazi wake akiwa salama,baada ya wazazi kumpata mwanao walijawa na furaha na kumshukuru Mungu kwa kuwaokolea mtoto wao.
Familia ilipokuwa ikifurahia kupatikana kwa mwanao na kusherehekea mshukiwa mkuu Joseph Murithi Kibutu alisalia korokoroni akifanyiwa ukaguzi na uchunguzi na mafisa wa Polisi huku akisubiri kufikishwa mahakamani kujibu mashitaka.
Ni tukio ambalo liliwaacha wengi vinywa wazi wakijiuliza maswali bila kupata majibu kuhusiana na jambo hilo, wengi wa wazazi walilaani kitendo hicho cha kinyama huku wakiwahongera maafisa wa usalama kwa kukuwa ange na kumwokoa mtoto huyo.
Vilele wengi walielezea hofu ya usalama wa Watoto wao
wakisema kuwa hilo tukio linaweka maisha ya familia nyingi katika hali ya wasiwasi
wakisema ipo haja ya jamii kushirikiana na kuwatambua watu walio na nia mbaya
kama ya bwana Murithi.