Maafisa wawili wa polisi wametiwa mbaroni huku uchunguzi ukianzishwa kwa tuhuma za kuhusika katika wizi wa kimabavu jijini Nairobi.
Idara ya DCI imeeleza kwamba maafisa hao wawili ndio washukiwa wakuu baada ya kufumaniwa katika shughuli za kumnyanyasa raia kwa usaidizi wa mhusika wa tatu katika mtaa wa Githurai.
Kulingana na repoti ya polisi, Maafisa wa usalama wa Gidhurai wakiwa kwenye shughuli zao za kawaida ndipo walipowafumania maafisa hao waliokuwa wakimuibia raia.
Waliwatia mbaroni wahusika hao ambao walitambulika kama maafisa wa usalama pamoja na muhusika wa tatu.
Watatu hao walikuwa wamemwangusha raia huyo chini wakiwa na nia ya kumuibia bidhaa zake' Tayari wamefikishwa kwenye kituo cha police cha Gidhurai wakingoja kufikishwa mahakamani.
Kulingana na kitendo hicho idara ya DCI imewaonya raia na maafisa wa usalama kushirikiana katika kuwaibia watu, idara hiyo imesisitiza kwamba vitendo kama hivyo vitachukuliwa na sheria kali sana.
Kitendo hiki kimetokea siku chache tu baada ya maafisa wa kitengo cha Serious Criminal investigation [SCU[ kwa kushirikiana na wengine kumutia mbaroni afisa ya DCI anayedaiwa kuhusika katika wizi wa kimabavu.
Afisa huyo wa DCI, kutoka Kibwezi Kaunty ya Makueni alishikwa siku ya Jumaa tatu Feburuari 17 kutokana na ushahidi unaomuhusisha na wizi wa kimabavu mwaka 2022'
Wakati wa wizi huo mhudumu mmoja alipigwa risasi tumbuni na kuaachwa akiuguza majeraha kabla ya mshukiwa kotoroka na shilingi elfu 50.
Maswala ya vyombo vya usalama kuhusika katika vitendo viovu vya kuwabia wananchi badala ya kuwalinda na mali zao vinaongeza wasiwasi miongoni mwa wananchi.
Hili ni jambo ambalo idara husika zinafaa kushugulikia kwa kina na kukomesha kabisa ili kuleta imani katika vyombo vya usalama kwa wananchi.