logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Kaunti za shutumiwa kwa kutengea maendeleo bajeti finye

Hazina Kuu ya taifa yakosoa serikali za Kaunti kwa kutenga mgao wa asilimia ndogo ya bajeti yao kwa ajili ya Maendeleo.

image
na Evans Omoto

Yanayojiri19 February 2025 - 10:46

Muhtasari


  • Kulingana na Ripoti iliotolewa na mkaguzi mkuu wa  hesabu ya serikali ilionyesha Kaunti nyingi nchini ambazo hazikutenga fedhaa nyingi kwa miradi ya maendeleo katika bajeti yake ya mwaka wa 2023/2024.
  • Kulingana na taarifa ya bajeti ya mwaka 2025/26 kwa jumla kaunti zote hazikufikisha kile kiwango ambacho kinahitajika kisheria.

Hazina ya taifa yakodolea macho serikali za Kaunti

Hazina Kuu ya taifa ilinyoshea kidole cha lawama serikali za Kaunti kwa kutenga mgao wa asilimia ndogo ya bajeti yao kwa ajili ya Maendeleo.

Kulingana na Ripoti iliotolewa na mkaguzi mkuu wa  hesabu ya serikali ilionyesha Kaunti nyingi nchini ambazo hazikutenga fedhaa nyingi kwa miradi ya maendeleo katika bajeti yake ya mwaka wa 2023/2024.

Ripoti iliyotolewa na hazina kuu ya taifa iliweza kurodhesha Kaunti mbalimbali kama zilie zilifeli kutenga asilimia kubwa ya pato la kaunti kwa ajili ya Maendeleo.

Baadhi ya Kaunti hizo ni Nairobi,Kisii  na Mombasa inasemekana hata baada ya kuwa na muongozo maalum kikatiba ambao unaowangoza magavana jinsi ya kutenga fedha ambapo sheria inaeleza na kufafanua vizuri kuwa miradi ya maendeleo katika Kaunti inastahili kutengewa asilimia 30% ya bajeti.

Nairobi kaunti ilitenga asilimia 10.3% kwa pato lake lote kwa ajili ya maendeleo,Kaunti ya Kisii ilitumia asilimia 13.7%,Mombasa asilimia 16.2%, Kisumu asilimia 17.5%,TaitaTaveta asilimia 18.6% na Kiambu 19.4%.

Kipengee cha kudhibiti mali ya umma cha mwaka wa 2012 huzipa na huzihitaji Kaunti angalau kutenga asilimia 30% ya pato lake kwa ajili ya maendeleo.

Hazina ya taifa ilisema kuwa ukaguzi wa utumizi wa pesa za umma kwa maendeleo kwa miaka iliopita 2021/22,2022/23 na 2023/24 ilirekodi asilimia 25,23 na asilimia 24 mtawalia.

Kulingana na taarifa ya bajeti ya mwaka 2025/26 kwa jumla kaunti zote hazikufikisha kile kiwango ambacho kinahitajika kisheria.

Zile Kaunti ambazo ziliongoza kwa kutenga angalau asimia kubwa ya bajeti yao kwa ajili ya maendeleo ni  Marsabit kwa asilimia 33.3%,Narok 34%,Homabay na Mandera asilimia 33.3% Siaya asilimia 32.6%,Trans Nzoia 31% Kitui 30.8%,Kilifi 30.6% na Turkana 30.6%.

Mwaka wa 2023/24 Kaunti zilitumia jumla ya shilingi bilioni 209.8 kwa matumizi ambapo ni kiwango sawa na  asilimia 47.6% kutoka kwa jumla ya shilingi bilioni 440.7 zilizokusanywa.

Kwa mara nyingi Kaunti zimekuwa zikitumia hela nyingi kwa kulipa mishara huku miradi na maendeleo ikitelekezwa ripoti ya mkaguzi wa bajeti ilieleza.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved