Gavana Sakaja apongeza programu ya lishe kwa watoto shuleni
Mpango wa programu ya lishe shuleni ambao ni mradi
ulioasisiwa na Gavana Johnson Sakaja ulipigiwa upato na kuonekana kuwa wa manufaa sana.
Programu hio ambayo ilipewa jina maarufu ‘Dishi na Kaunti’
ni programu ambayo ilikusudiwa kuwapa mlo wanafunzi wa shule za umma kwa gharama ya chini sana
katika maeneobunge kumi na saba(17) Nairobi.
Kutokana na kuanzishwa kwa mradi huu muhimu wa maankuli shuleni umechangia pakubwa kujengwa kwa jikoni kumi na saba na kuwaajiri wafanyakazi wengi katika mpango huo.
Huu mradi ni miongoni mwa miradi ambayo ilikuwa katika
manifesto ya Gavana alipokuwa akirai wananchi wampigie kura akisema kuwa ni
mradi ambao ulilenga shule za umma zote zikiwemo za chekechea.
‘’Dishi na Kaunti ni ndoto ambayo imekuja kutimia nikiwa
Seneta nilitamani sana kuona Watoto wakila shuleni kwa sababu nilibaini kuwa kati
ya watoto wanne mtoto mmoja hukosa kuhudhuria Vipindi vya masomo kisa na maana ya
ukosefu wa Chakula’’.
‘’Niliahidi kuwa iwapo nitachaguliwa ningeanzisha mradi huo
kwa haraka iwezekanavyo na kwa sasa ninaona hilo limetimia ambapo ni jambo zuri
la kujivunia’’Gavana alisema.
Kwa sasa mpango huo wa Dishi na Kaunti unalisha jumla ya Wanafunzi elfu mia tatu na Watoto kumi 310,000
nambari ambayo ni ya kujivunia na ambayo inaashiria mwanga wa maisha mema
kimasomo kwa wanafunzi wetu wawapo shuleni.
Mradi huu wa Gavana ulilenga kupunguza baa la njaa kwa
wanafunzi hasa wa mijini ili kuwapa nafasi sawa kimasomo na kupata elimu pasi kuwa na vikwazo vyovyote.
Gavana anapoendeleza mipango ya ajenda yake katika jiji kuu
la Nairobi hio ni baadhi tu ya miradi imara ambayo amekuwa akiendeleza ikiwemo
na shughuli ya kulisafisha jiji la Nairobi na kuwaondoa wachuuzi Katikati ya jiji
kuu.
Gavana awapo mbioni kutimiza ahadi zake alizowaahidi wananchi
wa Nairobi vilevile ameendeleza wito wa kuwa na ushirikiano kati ya maafisa wa
mamlaka inayosimamia shughuli na kuendesha mipango ya Nairobi na wananchi ili
kuwe na wepesi wa kutekeleza na kufanikisha shughuli za Kaunti pasi kuwa na mvutano wowote .