Jaji mkuu wa zamani Maraga ahimiza serikali kuzingatia Afya
Aliyekuwa Jaji mkuu David Maraga alielezea wasiwasi wake kuhusu hali mbaya inayoendelea katika
hospitali za umma nchini.
Katika chapisho rasmi aliloandika katika ukurasa wake wa X uliojulikana
kama twita jaji huyo wa Zamani
alisikitikia wito wa muungano wa hosiptali za binafsi wa kutaka kusitisha
huduma zake kwa wagonjwa kwa kisingizio cha serikali ya taifa kutolipa malimbikizi
ya madeni kwa hospitali hizo.
Maraga alisema kuwa kutozipa hela hospitali hizo hakustahiki
ikizingatiwa kuwa serikali i mbioni kuvumisha mfumo wa huduma za afya kwa jamii
kwa wote ambao unastahili kuwa
unawajibikia suala hilo pana.
Alisema kuwa Wakenya wengi walikuwa wakitoa pesa kwa huduma
za NHIF mwanzoni kabla ya kuhamia kwa huduma ya SHA alisema kuwa ni hatua ya wagonjwa
kunyimwa huduma za matibabu ambayo ni haki yao kimsingi haistahili.
Alikariri kuwa wagonjwa wengi huhitaji huduma za dharura
ikikusudiwa kuwa maradhi wanayokabiliwa
nayo hayawezi kusubiri kamwe.
Alitoa wito kwa serikali kuchukua hatua za haraka kusuluhisha
suala hilo na kuokoa sekta ya afya ambayo ni nguzo muhimu katika maisha ya
binadamu vilevile aliongezea akisema kuwa afya ni jambo la tija katika
maisha ya mja yeyote hivyo basi
linasitahili kushughulikiwa kwa dharura.
Alisema kuwa idara ya afya kutotoa huduma bora kwa umma
imetekwa na sheria mbovu ambazo
hazisaidii na vilevile ufisadi ambao umeshehemni na kumea zaidi .
Alisema kuwa kama taifa hatuwezi kuwa tunapiga hatua mbili
mbele na tunapiga hatua tano nyuma kimaendeleo kama taifa, kwa idara ya afya
linakuwa ni jambo la kufedhehesha sana kwa sababu ya watu wachache kupata nafasi ya kupora pesa
za umma.
Maraga alisema kuwa taifa ambalo lina watu wagonjwa haliwezi
kupiga hatua kimaendeleo na kufikia ruwaza inayolenga hivyo ni jukumu la
serikali kuhakikisha kuwa tiba katika nchi iko imara na ya kujivunia ipasavyo.
Kauli ya Maraga inajiri wakati ambapo madaktari
wanashinikiza serikali kuwalipa madaktari wanagenzi mishahara yao.