logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Habari zilizochapishwa katika magazeti kuwa Raila Odinga aliokoa nchi kutochuliwa na majeshi ni za uongo wizara ya ulinzi yasema

Wizara ya Ulinzi yakanusha taarifa zilizochapishwa katika magazeti ya Sunday Nation na Taifa leo kuwa Raila Odinga aliokoa Rais Ruto

image
na Evans Omoto

Yanayojiri17 March 2025 - 14:39

Muhtasari


  • Wizara ya ulinzi wa taifa  la Kenya ilitaja Habari hizo kama za uongo,hazina msingi,zizizokuwa na Mashiko ,Habari za Kupotosha na za kimzaha.
  • Kupitia kwa barua hiyo ujumbe ulizidi kueleza kuwa Wizara ya ulinzi ni taasisi ambayo ina maadili na ambayo ilijitolea kufanya kazi kwa heshima ,maadili na kutumikia taifa kwa haki,usawa na uwazi.

Wizara ya Ulinzi yakanusha taarifa zilizochapishwa katika magazeti ya Sunday Nation na Taifa leo kuwa Raila Odinga aliokoa Rais Ruto kutoka nchi kuchukuliwa na Jeshi kufuatia maaandamano ya vijana wa Gen -Z Ya kupinga msuada wa Fedha wa 2024-2025.

‘’ Wizara ya Ulinzi ingependa kukanusha na kusema kuwa taarifa zilizochapishwa katika magazeti ya vyombo vya Habari ya Sunday Nation na Taifa Leo mtawalia  yaliyokuwa na Mada nikinukuu RAILA: ‘’I saved Ruto  from Millitary Coup’’ na Gazeti la  Taifa Jumapili lenye mada  ‘’Nilivyozima Mapinduzi Dhidi ya Ruto’’.

Barua hio ilioeleza kuwa machapisho hayo  katika magazeti ya taifa hayakueleza na kufafanua vyanzo maalum vya madai hayo kuwa aliyekuwa Waziri mkuu wa Zamani Raila Odinga katika mahojiano yake na vyombo vya kuwa alizuia uongozi wa Rais Ruto dhidi ya kuchukuliwa na Majeshi.

Wizara ya ulinzi wa taifa  la Kenya ilitaja Habari hizo kama za uongo,hazina msingi,zizizokuwa na Mashiko ,Habari za Kupotosha na za kimzaha .

Kupitia kwa barua hiyo ujumbe ulizidi kueleza kuwa Wizara ya ulinzi ni taasisi ambayo ina maadili na ambayo ilijitolea kufanya kazi kwa heshima ,maadili na kutumikia taifa kwa haki,usawa na uwazi.

Jeshi la taifa litasalia kuwa imara na tiifu kwa Rais ambaye ni  amri jeshi mkuu wa majeshi yote ya taifa na liko imaara na tayari kwa kulinda taifa kwa hali  na mali  pasi kuegemea mirengo ya kisiasa au kuwa na masilahi ya binafsi.

Machapisho ya Taifa Leo na the Sunday Nation yalitoa taarifa zisizo za kweli na ambazo vyanzo vyake havithaminiki ifaavyo na  lengo la machapisho hayo yalikiuka uzalendo wa nchi na kujikita katika lengo la kuongeza idadi ya wasomaji huku  yakikwepa ustaarabu wa wanahabari inavyostahiki.

Hivyo wizara ya ulinzi ilitoa wito kwa mashirika ya vyombo vya Habari kuzingatia ukweli na maadili na vilevile usalama wa taifa haswa wanaporipoti masuala kuhusu usalama wa taifa  barua ilifafanua kwa undani zaidi.

Wizara ya ulinzi inatoa taarifa ya kukanusha madai haya siku moja baada ya  magazeti hayo kuchapishwa ambapo mhusika mkuu bwana Raila Odinga alihojiwa siku ya Jumamosi katika mahojiano yalifanyika nyumbani kwake Karen.

 


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved