Katikati ya mwezi huu Taifa la Kenya liliripoti kuhusu mkurupuko wa ugonjwa wa Kala -azar katika Kaunti ya Wajir.
Ugonjwa huo uliweza kusababisha vifo vya watu 18 na kuathiri
zaidi ya watu 500 katika kipindi cha miezi mitatu iliyopita.
Kala-azar ambao pia hujulikana kwa kimombo kama Leishmania
Parasite ni ugonjwa ambao huambukizwa na aina ya kimelea kwa jina mchwakichuguu na ambapo dalili zake ni kupoteza uzani na
kuongezeka kwa maini ya binadamu.
Zaidi ya kesi 532 ziliripotiwa huku wagonjwa mbalimbali
wakipona baada ya kutibiwa .
‘’Tunapambana na mkurupuko wa ugonjwa kwa hivyo tunaomba
wananchi waweze kupokea matibabu kwa haraka kuzuia vifo’’. Daktari Ali Kutoka hospitali kuu ya
rufaa ya Wajir alisema.
Kulingana na dalili za shirika la afya Duniani WHO lilisema
aina hio ya ugonjwa wa Leishmaniasis huweza kusababishwa na aina ya vimelea
zaidi ya 20 na zaidi ya mchwakichuguu 90 huweza kusambaza ugonjwa huo.
Ilisemekana kuwa ugonjwa aina ya Kala-azar ni ugonjwa hatari
ambapo ukiwachwa unaweza kusababisha vifo na kuleta madhara makubwa , ikisemekana
kuwa zaidi ya jumla ya kesi asilimia 95 hazijatibiwa wala kushughulikiwa.
Visceral
Leishmaniasis-Ugonjwa huo mara nyingi umeripotiwa katika nchi ya Brazil,Afrika
Mashariki na sehemu za India ikikadiriwa kwa jumla ya kesi 50,000 hadi 90,000 kulingana na kesi ambazo zimeripotiwa katika
deta za WHO.
Cutaneous Leishmaniasis- ni aina ya pili ya dalili za
ugonjwa wa Kanal-azar ni ugonjwa ambao huenea sana na husababisha mchibuko wa Ngozi
na ugonjwa wa vidonda vya tumbo na
kuwashwa kwa sehemu za mwili kwa ukali zaidi,
sampuli ya ugonjwa huo hutokea sehemu za Marekani, mto meditereniani na
katika nchi za milki za kiarabu. Ambpo zaidi
ya Kesi 600,000 hadi milioni moja huweza
kushuhudiwa.
Leishmamia parasites- ni aina ya maradhi ambayo husambazwa
kutokana na kuumwa na aina ya mchwakichuguu aina ya kike ambaye hufyonza damu ili kutaga mayai ambapo katika kitovu chake cha kufyonza damu
ni asilimia 70 ya damu za Wanyama ikiwwemo damu ya binadamu.