Mkaazi wa Nakuru anashurutisha Gavana Kihika kurudi nyumbani baada ya kudaiwa kukaa sana katika taifa la Marekani.
Katika barua kwa rais wa Marekani Donald Trump na kwa Rais wa Kenya William Ruto Evans Kimori katika barua yake alisema kuwa taifa la Marekani lifanikishe kurudi kwake nyumbani ili aendeleze majukumu yake kama Gavana.
''Kwa niaba ya watu wa Nakuru kwa heshima ninaomba uingilie kati kwa kuhakikisha kuwa Bi Kihika anarudishwa nyumbani Kenya ili aendeleze shughuli zake za kikazi,'' barua ya Bwana Kimori ilisema.
Alisema kuwa wakazi wa Nakuru wanahitaji uwajibikaji wa uongozi hata hivyo walisisitiza kuwa kutokuwepo kwa Gavana Kihika kunawanyima haki ya kupata uongozi mwema kutoka kwa wapiga kura.
Vilevile Kimori alimkashifu Bi Kihika kwa kuifunga Hospitali ya War Memorial ambayo alisema iliwaacha mamia ya wakazi wa Nakuru bila huduma za afya njema jambo walilokuwa wakipata hapo mwanzoni.
Alisisitiza kuwa kuendelea kukaa kwa Gavana Kihika Katika Taifa la Marekani ni kuashiria kuwa anakwepa majukumui yake ilihali anaendelea kupokea mshahara mnono kutoka kwa walipa ushuru wa Kenya hasa wakazi wa Nakuru.
''Kama kiongozi aliyechaguliwa kama Gavana ana haki ya kikatiba kuhakikisha kuwa anafanyia kazi wananchi waliomchagua kazi kama vile Huduma za afya ambayo ni tija kuu kwa wananchi ilihali yeye kukaa kwake sana Marekani ilihali huduma muhimu zinaendelea kuyumbayumba inaonyesha ukiukaji mkubwa wa kazi kwa wananchi ilihali anaendelea kupata mshahara mkubwa''. Bwana Kimori alilama katika barua yake.
Wakati ambapo chapisho hili lilikuwa linachapishwa hakukuwa na majibu kwa barua ya bwana kimori kutoka kwa wahusika waliotajwa katika barua rais TRUMP NA RUTO ilihali Gavana mwenyewe alionekana akituma miradi ya maendele,o inayoendelea katika gatuzi lake la Nakuru.
'' Kwa siku chache zilizopita tumeendelea kutoa huduma za maendeleo kwa kuangazia miradi mbalimbali ya Maendeleo ya maji na kuendeleza ustahimilivu wa hali ya tabianchi kupitia kwa kufadhili mradi wa tabianchi wa FLLOCA ''. bi Kihika alieleza.
Mnamo Machi 11,2025 Milicent Omanga aliwahi tuma picha ya wao wakiwa wawili ila hakufafanua wala kusema zaidi ni wapi walipokuwa na walikuwa wakifanya nini.