Rais William Ruto mesema kwamba Waziri wa utumishi wa umma na ambaye pia alikuwa mwanasheria mkuu wa serikali Justine Muturi alikuwa hawezi kazi
katika enzi zake.
Rais alipokuwa akiwahutubia waisalamu katika ikulu ya
Nairobi siku ya Jumanne 25 Machi ,2025 katika hafla ya sherehe za ifutari Rais alikuwa akijibu swali
ambalo jamii hiyo ilikuwa imerai serikali kuwezesha fedha za kuanzisha wakfu Pamoja na kuidhinishwa rasmi
katika dini hiyo.
Katika jawabu lake Rais Ruto aliweza kusema kuwa ombi walilokuwa
wamependekeza litekelezwe kwa jamii ya waislamu lilikuwa linataka liweze kutolewa
kwa kutiwa sahihi na mshauri mkuu wa serikali kama njia mojawapo ya hitaji la
Kisheria.
Rais aliwaomba radhi kwa kusema kuwa mpango huo ulicheleweshwa
kwa sababu aliyestahili kutekeleza wajibu huo kama kiongozi alikuwa hana uwezo
wa kutekeleza kazi vyema.
‘’Tunapoendelea kusonga
mbele kwa kuangazia masuala ya elimu jinsi ambavyo mmesema na vilevile
kuangazia suala kuu la kuhusu kupata wakfu kwa hakika ni jambo ambalo limekawia sana kwa kuchukua
muda mrefu ila mniwie radhi kwa hilo kwa
sababu nilikuwa na mshauri mkuu wa serikali ambaye alikuwa hajui kazi
ipasavyo lakini kwa sasa nina mwanadada
ambaye anachapa kazi kwa uzuri hivyo tutatekeleza’’.Rais Ruto alisema.
Mzozo kati ya Waziri wa utumishi wa umma bwana Muturi na
serikali ulianza tu pale ambapo kulishuhudiwa maandamano ya vijana wa kizazi
cha Gen Z mwaka jana Juni wakati ambapo kulishuhudiwa maandamano ya kupinga mswada wa Fedha wa 2024/2025.
Katika kipindi hicho kulieza kushuhudiwa vijana wengi
wakitekwa nyara ili kuweza kutuliza hali tete iliyokuwepo enzi hizo na katika
harakati hizo mtoto wa aliyekuwa mshauri mkuu wa serikali na ambaye ni Waziri wa
utumishi wa umma kwa sasa Justine Muturi aliweza kutekwa nyara.
Miezi sita baadaye Bwana Muturi alijitokeza katika vyombo
vya Habari na kuanza kuikashifu serikali kwa kuweza kuwa katika njama ya
kumteka mwanawe pasi sababu zozote wala kumuwasilisha mahakamani kwa makosa ya
kutekwa nyara.
Tangu hapo kumekuwa kukishuhudiwa vita vya maneno baina ya Waziri
Muturi na serikali huku akiwa mstari wa mbele kulaani tabia inayoendeshwa na
serikali pasi kuwaajibisha wahusika wa utekaji nyara.