Wakazi wa mtaa wa Eastleigh katika kichochoro cha Athuman Kipande alimarufu Jam street walikadiria hasara kubwa baada ya maduka yao kubomolewa.
Ni shughuli ambayo iliendeshwa na trekta za mamlaka ya usimamamizi wa Kaunti alimaarufu Kanjo kwa kile kilichosemekana kuwa watu walikuwa wamejenga vibanda kando ya barabara ambavyo vilisababisha msongamano wa magari na watu kila uchao.
Kulingana na duru za kuaminika iilisemekana kuwa mfanyabiashara mmoja mashuhuri katika mtaaa huo alikuwa ametoa ilani kwa usimamizi wa Kaunti kuweza kuwaaondoa wachuuzi ambao wako karibu na jumba lake la biashara ambalo huuzia wateja wake kwa maauzo ya Jumla .
Ilisekana kuwa ilani ilikuwa imetolewa ya kuwamuuru wachuuzi na wafanyabiashara hao kuweza kuondoka ili kupisha biashara za wenyewe kuweza kuendelea bila usumbufu na vilevile kuhakikisha kuwa usafiri hautatiziki.
Kulingana na usimamizi wa muungano wa wafanya biashara katika eneo hilo la Eastleigh EBDA (Eastleigh Business District Assocition) ukiongozwa na mwenyekiti wake Omar Abdi alisema kuwa walikuwa wametoa notisi ya kuwaarifu wafanyabiashara ambao wanaendesha shughuli za biashara kando ya biashara kuwa waondoke ili kurahihisha njia ya usafiri pamoja na nafasi ya malori kupakia na kupakua mizigo bila matatizo.
''Kuna wafanyabiashara waliojenga kando ya barabara na vilevile kuna bodaboda wengi wanaosimama hapa kwa barabara kwa ajili ya kuendeshea biashara zao hapa ila wanasababisha msongamano wa magari pamoja na watu kwa kiwango kwamba magari ya kuleta mizigo yanakosa mahali pa kusimama yakishukisha na kupakia mizigoo na kuwa ni vigumu kwa sababu ya idadi kubwa ya watu''.Omar alisema.
Hata hivyo mwenye jumba kuu la bishara maeneo hao la bishara alikuwa ametishia kuichulia serikali ya Kaunti ya Nairobi hatua ikiwa haingechukua hatua ya kuwaondoa wafanyabiashara hao katika maeneo hayo.
Baadhi ya aina za biashara zilizopata kuathika ni biashara mbalimbali za buchari,maduka ya vifaa vya kielekroniki,maduka ya nguo , maduka ya mboga na matunda, vinywaji na maduka ya manukato mbalimbali. ''
''Mimi nililala nikiwa na kila kitu changu duka langu nilikuwa nimeongeza na kununua bidhaa zinazokadiria shilingi millioni kumi lakini nimeamuka nikakuta sina chochote mali yangu yote imeharibiwa'' Ahmed Jilious mfanyabiashara EASTLEIGH alisema.
Jumla ya maduka 5200 yaliweza kuharibiwa huku wenyewe wakiachwa hoi wasijue la kufanya wala pa kukimbilia.