Raila Odinga akanusha vikali kuwa chama chake cha ODM kuwa ndani ya serikali akisema kuwa aliipa serikali wataalamu wa kuchapa kazi.
Odinga alizungumza hayo akiwa katika matanga ya marehemu Julius Laban Murungi Kule Meru ambaye ni babake Betty Murungi Orengo ambaye ni mkwe wake Gavana wa Siaya James Agure Orengo.
Katika hafla hiyo bwana Odinga aliweza kufafanua wazi kwa kusema kuwa yeye pamoja na chama chake hawako katika serikali ya KENYA KWANZA bali waliweza tu kushirikiana nayo kwa manufa ya ustawi wa taifa.
Odinga aliweza kusema kuwa kutokana na wimbi lililokuwa likikabili serikali ya Kenya Kwanza kutokana na maandamano ya vijana wa kizazi cha Gen z ni baadhi ya sababu kuu zilizofanya ajitolee aisadie serikali ya Kenya kwwanza na wataalum wa kazi ili taifa liweze kusonga mbele.
''Wakenya walisema Ruto ni Lazima aende, wakapinga mswada wa fedha wa 2024/2025 hatimaye alikuja akawasikiliza na kuvunjilia mbali baraza lake la mawaziri hatimaye aliniomba nimpe wataalamu wa kazi, tumemsaidia tu Chama cha ODM hakipo kwa serikali , Mimi si waziri katika serikali ya Ruto''. Odinga alieleza.
Shinikizo hizo zilizidi kutolewa kutokana na chama hicho cha ODM kuweza kutoa zaidi ya mawaziri watano John Mbadi wa Fedha,Dorcas Oduor mshauri mkuu wa serikali, Opiyo Wanayi waziri wa Nishati,Wycliffe Oparanya waziri wa Mashirika na biashara ndogondogo na Hassan Joho Waziri wa madini na uchumi wa majini miongoni mwa makatibu wakuu katika wiraza mbalimbali walioteuliwa muda mchache uliopita.
Hata hivyo kutokana na uwepo wa wafanyakazi hawa kutoka ODM ndani ya serikali ndio uliochochea watu kuamini kuwa ODM iko katika serikali ya Kenya Kwanza na hivyo kuwa inacheza karata mara mbili kuwa katika serikali na kwa wakati huo kusema wako upinzani.
Kiongozi wa Chama cha People Liberation Party Martha Karua ambaye pia alikuwa muwaniaji mwenza wa Odinga katika Uchaguzi uliopita wa 2022 alimkashifu Odinga kwa kuwa ndumakuwili kuwa ndani ya serikali na vilevile kujidai kuwa wako upinzani.
Aliweza kusema kuwa itakuwa vyema kama Serikali ya Kenya kwanza na ODM watafika katika afisi za msajili wa vyama ili waihalalishe ndoa yao rasmi ili kusiwe na mchanganyiko unaoshudiwa nchini hata mpaka kwenye bunge la Taifa ambapo mahakama ilitoa uamuzi kwa kusema kuwa mrengo wa Azimio ndio ulio na idadi kubwa ya Wabunge jambo ambalo Spika wa bunge la Taifa Moses Masika Wetangula alisusia kutii agizo hilo hadi sasa.