Seneta wa Muranga Joe Nyutu amedai kuwa aliyekuwa Naibu wa Rais wa Ramani Rigathi Gachagua alikuwa amewapanga wakaazi wa Mlima Kenya kuhusu ujio wa Rais Ruto Mlimani..
Katika maelezo yake Bwana Nyutu alisema kuwa Gachagua alikuwa tayari amewaelezea wakaazi wa Mlima Kenya kuhusu uwezekano wa Rais kuweza kuwashawishi wakazi wa mlima kenya kwa kuwaelezea maneno matamu kuhusu ziara yake ambayo alikuwa amekusudia kuitekeleza.
'' Naibu wa Rais wa pili bwana Rigathi Gachagua alikuwa amewashauri watu wetu kuwa kulikuwa na pesa ambazo zilikuwa zinasitahili kupelekwa kwa wizara ya Elimu, wizara ya afya(SHA),na kuwapelekea watoto wetu Nyumbani lakini hizi pesa zimegeuzwa kutoka kwa kushughulikia vitu muhimu''.Nyutu alisema.
''Tuliwashauri kutochukua hela chache kwa sababu kulikuwa na zawadi ya pesa nyingi ilikuwa inawangoja kwa kuhudhuria mikutano zawadi ya kupiga makofi na kutabasamu na hivyo ndivyo Rais Ruto alivyofanya.'' Seneta Nyutu alieleza.
Matamshi ya Nyutu yanajiri wakati ambapo Kiongozi wa taifa kwa sasa anaendeleza ziara yake kwa siku ya Tatu akiwa katika eneo pana la Mlima Kenya kwa ajili ya uzinduzi wa miradi mbalimbali ya maendeleo.
Rais siku ya leo anatarajiwa kuzuru Kaunti ya Nyandarua na hatimaye kufululiza moja kwa moja hadi kaunti ya Muranga kwa msururu wa kuzindua miradi mbalimbali ya maendeleo.
Itakumbukwa wazi kuwa kabla Rais aanze ziara yake Mlimani aliyekuwa Naibu wa Rais Rigathi Gachagua alikuwa amewarai wakaazi wa Mlima Kenya Kumuuliza rais ni maendeleo gani aliokuwa anaenda kuzindua ilihali barabara nyingi na miradi mingi ilikuwwa imekwama.
Vilevile Naibu huyo wa rais alikuwa amekisia kuwa kutokana na kuondolewa kwake katika serikali wakaazi wa Mlima Kenya walikuwa hawana imani na rais kwa kiwango kikubwa hivyo alikuwa ametoa madai kuwa wananchi wangelipwa pesa nyingi ili waweze kuhudhuria mikutano yake.
Lakini kinyume cha matarajio ya wengi tangu wakati ambapo rais alipotua katika eneo hilo hasa kaunti ya Laikipia na Nyeri wananchi wengi walijitokeza kushiriki na kuhudhuria mikutano yake huku wakimshangilia kwa shangwea na nderemo.
Hata mwandani wa karibu wa Rigathi Gachagua bwana Mutahi Kahiga gavana wa Nyeri alikuwa mstari wa mbele kumpokea rais kwa mikono miwili.