Siku ya Rais Ruto alizuru Kaunti ya Nyandarua kwa ziara ya uzinduzi wa miradi mbalimbali ya maendeleo..
Akiwa katika eneo la Ol Kalou, kaunti ya Nyandarua, Rais aliweza kuzungumza na wananchi ambao walimkaribisha kwa shangwe.
Katika usemi wake Rais aliweza kuwapongeza wakaazi wa Nyandarua kwa kukuwa wangwana na wenye uvumilivu sana.
Aliweza kuwahakikishia kuwa serikali ilikuwa mbioni kuhakikisha kuwa kila jambo linakuenda kwa uzuri bila kutatizika wala kuchelewa. Rais aliweza kutoa ahadi na hakikisho kuwa miradi yote iliyokuwa imekadiriwa kukamilika ilikuwa katika shajara yake.
Rais aliweza kuzindua chuo kikuu cha Nyandarua ambapo alisema ifikapo mwezi wa tisa wanafunzi mbalimbali watakuwa wanajiunga na chuo hicho ili kuhakikisha kuwa elimu inaendelezwa ipasavyo.
Vilevile Rais aliweza kuzindua masoko yaliokuwa yamejengwa katika Gatuzi hilo kwa kuwahakikishia wananchi kuwa bidhaa zao kutoka mashambani zingepata mauzo kwa haraka kwa sababu ya uwepo wa masoko ya kutosha.
Aliweza kuzindua masoko kumi kwa ajili ya faida ya wananchi ambao walikuwa wakulima hodari na waliokuwa wamekosa mahali pa kuuzia bidhaa zao.
Rais Ruto aliweza pia kuzungumzia kuhusu ukarabati na ukamilishaji wa barabara kadhaa eneo hilo huku akidokeza kuwa barabara nyingi zilikosa kukamilika ni kwa ajili ya kutengewa bajeti fichu ila akasema kuwa kwa ushirikiano wa kaunti na serikali kuu barabara hizo zitatamatika haraka.
Rais pia aliweza kusema kuwa waliopewa majukumu ya kutekeleza na kufanya mambo kwa ustaarabu kwa muda wa miaka mitano kwanzia kwa diwani hadi kwa rais na iwapo baada ya kipindi hicho kama kila mtu hatakuwa ametekeleza wajibu wake ipasavyo hawatakuwa na budi ila kutumwa nyumbani na wananchi.
Kwa upande wake naibu wa Rais Kithure Kindiki aliwashukuru wananchi kwa kumkaribisha rais na kusema kuwa alikuwa akifanya hima kuhakikisha kuwa kila jambo linaenda kwa uzuri hasa kwa wananchi kwa kile ambacho alikitaja kama ushirikiano na umoja wa wananchi.
Kithure Kindiki aliweza kusema kuwa wale ambao walikuwa wakijaribu kumlazimisha ili aweze kupingana na rais aliwaambia kuwa yeye hatafanya hivyo na baadala yake atahakikisha kuwa anamsaidia rais kuendeleza maendeleo kwa wananchi bila ubaguzi wala ushindani.