Serikali imetangaza azma yake ya kukata rufaa kutokana na uamuzi wa mahakama kuu ya kusitisha malipo katika mfumo wa E-citizen katika shule .
Katibu mkuu katika wizara ya elimu Julius Bitok alisema hayo Jumatano alipokuwa katika mtaa wa Mukuru kwa Njenga walipokuwa wakizindua mradi wa madarasa mapya manane pamoja na mijengo mingine mitatu.
Mradi huo uliweza kufadhiliwa na serikali ya Merekani kupitia kwa wizara ya ulinzi kwa ushirikiano na serikali ya Kenya kupitia kwa wizara ya elimu kwa programu ya Endeleza elimu katika Jamii.
Katibu Bitok Katika hotuba yake aliweza kuihongera serikali ya Marekani kupitia kwa balozi wake hapa nchini Marc Dillard ambapo takribani shilingi milioni 84 ziliweza kutolewa kufadhilimpango huo.
Kutokana na mchango huo kulipa nafasi idara yetu ya elimu kuweza kuimarisha misingi yake na kuhakikisha kuwa kila kitu kinakwenda kwa uzuri na kwa manufaa ya wanafunzi na jamii kwa jumla.
''Maisha yetu ya siku za baadaye yanategemea elimu ya watoto wetu,kwa hivyo ushirikiano wetu na mashirika kama haya ambayo tunafurahia siku ya leo yanafaa kuwekwa juu kwa manufaa ya kusaidiana katika kila upande, kufikia sasa serikali ya taifa imejenga zaidi ya madarasa 16,000 ya gredi ya 9 kote nchini, Shule hii ya Kwa Njenga ni moja kati ya shule zitakazokuwa miongoni mwa shule bora nchini''.Bitok alisema katika hotuba yake.
Hata hivyo mpango huo ulipokuwa ukiendelea bwana Bitok aliweza kutoa tangazo kuwa serikali kupitia kwa wizara ya elimu itafika mahakamani kwa ushirikiano na afisi ya mshauri mkuu iili kuweza kukata rufaa kutokana na uamuzi wa mahakama kuu kuweza kusimamisha ulipaji wa Karo kwa kutumia mfumo wa E-CITIZEN.
Siku ya Jumanne jaji Chacha Mwita wa mahakama kuu aliweza kutoa uamuzi wa kusitisha ulipaji karo kwa kutumia mfumo wa e citizen Jaji alisema kuwa hakukuwa na ushirikishi wa umma ipasavyo kabla ya kuafikia kiwango cha utekelezaji wake.
Itakumbukwa wazi kuwa aliyekuwa katibu mkuu wa wizara ya elimu Belio Kipsang alikuwa ametoa mwongozo kwa shule zote kuwa zifanye malipo kwa e -citizen.