
Gachagua alidai kuwa Mwanablogu Dennis Itumbi na msaidizi wa kibinafsi wa rais bwana Farouk Kibeti ndio wanaoendesha serikali.
Gachagua alizungumza hayo alipokuwa katika mahojiano mnamo Aprili 7, 2025 alipokuwa akihadithia utendakazi wao katika serikali.
Gachagua alidadavua kwa kusema kuwa mara kwa mara viongozi hao walikuwa wakishiriki katika uwendeshji wa serikali katika masuala mengi.
Gachagua alisema kuwa katika mikutano mingi inayofanyika ikuluni mwanablogu Dennis Itunmbi hushinda akiwa karibu na ikulu huku akisikiliza kile ambacho huwa kinazungumziwa.
Gachagua alisema kuwa iwapo au ahisipo kuwa mazungumzo hayo hayachukui mkondo mzuri yeye huingilia kati na kuamuru rais kuwa wakati wake ulikuwa umeisha hivyo alikuwa anahitjika katika mkutano mwingine.
''Dennis Itumbi hushinda pale ikulu mnapokuwa na mkutano na rais halafu asikie mazungumzo yenu hayaleti shangwe utamuona akimwambia rais kuwa muda wako umeisha unastahili kuwa na mdahalo mwingine'' Gachagua alieleza.
Ukiona habari zozote ambazo viongozi mbalimbali huwa wanatoa katika vyombo vya habari au kusema ni mambo ambayo huwa yameandikwa na Dennis itumbi, hata ule ujumbe ambao ulisemwa na DCI kuhusu masuala ya vurugu kanisani hiyo yote ni kazi ya Itumbi''Gachagua alisema.
''Kisha kuna huyu mwingine kwa jina Farouk Kibet yeye naye huogopewa na kila mfanyakazi wa serikali kila maafisa wa serilkali huweza kuripoti kwake ukitaka kumwona Rais ni lazima Faroiuk ajuwe hata mkuu wa mawaziri MusaIia Mudavadi si kakatibu na viongozi wengine wengi huweza kujiwasilsha kwake mwanzo''.Gachagua alielezea.
''Yeye ndiye hupanga watu kule ikulu, mimi alikuwa anataka kunipanga nikakataa nilisema la siwezi kubali kupangwa na ndio maana unaona nilionekana kama mbishi na mbaya serikalini. '' Gachagu alifafanua.
Bwana Gachagua aliweza kuelezea mambo mengi kuhusu makosa ambayo yapo katika serikali hio ya Kenya kwanza
Aliweza kusema kuwa kitendo cha bwana rais kumfuta kazi Moses Kuria na kuja tena kumpa kazi ya kuwa mshauri mkuu wa rais alikisawiri kitendo hicho kama kumfukuza mchumba wako na hatimaye kuja kumchukua kama yaya tena ambapo ni madharau kwake.
''Rais kufuta kazi Moses Kuria ya uwaziri na badala yake kumpa mtu kama Kavogo huo ni upuzi kavogo ni mbumbumbu ilihali Kuria ni mwerevu kupindukia. Gachagua alisema.