
Kiongozi wa chama cha TWA Third Way Alliance Ekuru Aukot amesema kuwa kiongozi ambaye amekuwa uongozini kwa muda mrefu nchini ni Rais William Ruto.
Aukot alikuwa akizungumza katika mdahalo mzima wa hali halisi ya taifa katika idhaa ya Runinga ya Citizen mnamo Jumanne Aprili 8,2025 wakati alipotoa hoja hiyo kwa kusema kuwa rais Ruto ndiye kiongozi ambaye amekuwa kwenye madaraka ya uongozi kwa muda wa miaka 28 sasa.
Aukot alidokeza hayo akisema kuwa Tangu Ruto achaguliwe mnamo mwaka wa 1997 kama mbunge wa Eldoret Kasikazini amekuwa katika nafasi za uongozi kutoka idara moja hadi nyingine hadi kufikia leo.
Ila licha ya kuwa katika uongozi kwa kipindi cha muda mrefu Aukot alimshutumu kwa kusema kuwa hajakuwa akitumia nafasi yake vyema katika uongozi kuweza kusaidia raia ili waweze kujiendeleza na wao.
Aukoti alimkashifu Rais Ruto kwa kusema kuwa sifa na umaarufu ambao amekuwa akijizolea kila wakati na kupata heshima kuu hamna chochote cha kujivunia kutoka kwa raia na baadala yake Ruto amekuwa akijihusiaha tu na sifa za kutaka kupata utajiri.
''Ruto ndiye kiongozi ambaye amewahi kuwa kwenye safu ya uongozi kwa muda wa miaka mingi yule ambaye yuko hai baada ya marehemu rais wa Zamani Mwai Kibaki lakini licha ya hayo yote hamna chochote chenye ametekeleza kwa huo muda wake wote ambacho umma utajivunia'' Ekuru Aukot alisema.
''baadala ya kuchukua fursa hiyo ya kuwa na rekodi nzuri ya uongozi kuweza kufanya mambo ambayo yanashabihiana na rekodi yake mamlakani yeye amekuwa tu mstari wa mbele kutaka kujilimbikizia utajiri ili awe miongoni mwa wale mabwenyeye katika taifa'' Aukot alizidi kuelezea.
Aukur Aukot ni wakili na vilevile ni mmoja wa wasisi waliokuwa katika jopo lililoandika katiba yetu ya kenya ya mwaka wa 2010 na vilevile yeye ni kiongozi wa chama cha Third way alliance.
Ekuru Aukot aliwahi shiriki katika uchaguzi wa mwaka wa 2017 kama mwaniaji wa urais kupitia kwa tiketi ya chama chicho hicho chake cha Third Way alliance .