logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Gachagua asema uhuni wa mwaka 2007 Makanisani unajirudia

Rigathi Gachagua alisema kuwa maovu yaliotendeka miaka ya nyuma ya 2007 na 2008 yanajitokeza tena mwaka huu.

image
na Evans Omoto

Yanayojiri08 April 2025 - 08:09

Muhtasari


  • Gachagua alikuwa akihojiwa na kituo cha Runinga cha KTN nyumbani kwake Karen mnamo Jumatatu 7 Aprili, 2025.
  • Gachagua alisema kuwa mnamo mwaka wa 2007 baada ya uchaguzi mkuu  na kulitokea machafuko ya ghasia za kikabila ambapo watu wengi waliweza kupoteza makao halikadhalika na maisha yao.
Rigathi Gachagua

Aliyekuwa naibu wa rais Rigathi Gachagua amesema kuwa maovu yaliotendeka  miaka ya  nyuma ya 2007  na 2008 makanisani yanajitokeza tena  mwaka 

Gachagua alisema kuwa mnamo mwaka wa 2007 baada ya uchaguzi mkuu kulitokea machafuko ya ghasia za kikabila ambapo watu wengi waliweza kupoteza makao halikadhalika na maisha yao.

Gachagua aliweza kusema kuwa kulitokea magenge ya wahuni mwaka wa 2007/2008 waliokuwa wakiwauwa watu na kuwakatakata na vilievile kuchoma makazi yao kama vile tukio lililotokea katika kanisa la Kiamba ambapo watu wengi waliweza kuuwawa kwa kuchomwa moto.

Gachagua alikuwa akisimulia kisa hicho cha kumbumbuku ya zamani kwa  kuweza kuvuta taswira na kurejelea hali  halisi ya matukio yaliofanyika katika eneo la  Kasarani  alipokuwa akihudhuria ibaada  ya maombi  katika  kanisa la PCEA Mwiki siku ya Jumapili ya tarehe 6 Aprili ,2025. 

Mnamo Jumapili ya tarehe 6 Machi,2025 Gachagua akiwa katika kanisa la PCEA Mwiki Kasarani kulitokea kundi la vijana waliovamia waumini kanisani na kutaka kusambaratisha ibaada iliyokuwa ikiendelea na vilevile kutaka kulipwa hela  kwa lazima.

Gachagua alikuwa ni mwingi wa masikitiko akijutia kwa kusema kuwa anashangaa kuona matukio yaliyofanyika zaidi ya  miaka kumi na tano  iliyopita ikijirudia tena ya visa  vya uhalifu na ugaidi makanisani.

''Mwanzo nina masikitiko makubwa  sana kuweza kushuhudia matukio tulioona ya mwaka  wa 2007 na 2008 ya uhalifu wa watu  kuvamiwa makanisani  ambapo watu wengi sana waliweza kuuuwawa kwa kuchomwa moto wakiwa kanisani Kule Kiamba'' Bwana Gachagua alisema.

'' Katika tukio  hilo kulikuwa  na akina mama  na watoto wao wakati ambapo wahuni hao waliwavamia na kwa kuwa  wanataka kuwauwa wakiwa kanisani wale kina mama waliweza kuzai kwa kusema kuwa ni vyema wao wauawe na ilihali waache watoto wakiwa hai ila walisusia  na kuweza kuwasha moto na kuchoma kanisa  zima watu wakiwa  ndani huku watoto hao wakirushwa ndani kupitia kwa  madirisha''.Gachagua alieleza.

Gachagua aliweza kusema hayo akirejelea tukio lililomtendekea akiwa Mwiki Kasarani akihudhuria ibaada alisema kuwa kwa kufanya hivyo wanawakumbusha wale waliokumbwa  na machafuko hayo kuwa uhasama wa kijamii na vita makanisani vingalipo  jambo ambalo aliomba serikali kutoruhusu kwa vyovyote vile.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved