Evance Kamange, mbunge wa chama cha Mapinduzi Tanzania CCM, ameweka wazi kuwa wabunge wengi wa CCM waliingia bungeni kwa kutumia Rushwa.
Kamange alikuwa akizungumza na mwanahabari Chief Odembo Aprili 14,2025 alisema kuwa katika uchaguzi wa mwaka wa 2020 katika uchaguzi wa mchujo wabunge wengi wa CCM hawakupita kwa haki.
Kamange aliendelea kwa kusema kuwa katika kipindi hicho cha uchaguzi wa mchujo wabunge wengi walitumia pesa zao kuweza kujinyakulia nafasi za uongozi kwa sababu kulikuwa na idadi ndogo ya wapigakura ambao hawangewawezesha kujinyakulia ushindi wa moja kwa moja.
''Mwaka wa 2020 katika uchaguzi wa chama cha ndani uligubikwa na rushwa mimi mwenyewe nilikuwepo na nilishuhudia hilo , kuna baadhi ya wabunge ambao walichukua uongozi ambao hawana maono ya kumtetea mwananchi na kuweza kutekeleza mambo kwa faida ya mwananchi.
Baadhi ya wabunge walichaguliwa tu kwa ajili ya uwezo wao wa hela na walizidi kumpongeza rais badala ya kujenga mifumo miema ya kuweza kumsaidia mwananchi wakiwa kule bungeni ili waweze kuangazia matatizo ambayo yalikuwa yakimsonga mwananchi mpiga kura.
Kwa mfano wewe kama mbunge unastahili kuwa na akili pevu tena tambuzi ya kuweza kuwa na uongozi mwema ambao wapiga kura waliokuchagua ni kwa ajili ya kuwasilisha miswada kule bungeni ya kumtetea na kumlinda mwananchi wa kawaida lakini miongoni mwa viongozi hawa waliochaguliwa hawana wazo hilo wala uwezo wa kulandana na mabadiliko ya kileo katika kuandaa miswada mbalimbali'' Kamange alieleza.
Unajihisi vipi wewe kama kiongozi ambaye alichaguliwa katika chama tawala cha CCM ila unahisi kuwa mmoja yule ambaye ulichaguliiwa kwa misingi au kwa nguvu za hongo pamoja na wabunge wengine?
'' Kwa hakika sihisi vibaya ila ninataka kuwa mhimili wa mabadiliko katika uongozi wa chama cha CCM kwa hivyo ninataka kuwa kiongozi wa mabadiliko katika uongozi wa kisisa hivyo mabadiliko ya shareia za chama ni mazuri ili kuzingatia haki na ukweli pia ni jambo jeme.''
Matukio hayo yanajiri muda mchache wakati amabapo chama cha upinzani cha chadema kilipigwa marufuku kuweza kushiriki katika uchaguzi mkuu wa mwaka wa 2025.