Aliyekuwa naibu wa Rais Rigathi Gachagua aliandika barua ya kusema kuwa maisha yake yalikuwa hatarini na alihitaji kurejeshewa maafisa wake wa ulinzi.
Gachagua aliandika barua hiyo mnamo APRILI 15 , 2025 iliyoelekezwa kwa inspekta mkuu wa polisi bwana Douglas Kanja.
Kulingana na bwana Gachagua alisema kuwa kulingana na kuondolewa kwa usalama wake alisema kuwa maisha yake yalikuwa hatarini pamoja na familia yake na wafuasi wake.
Alisema kuwa kulingana na hitaji la katiba ya Kenya kila mtu ana haki ya kulindwa pamoja na mali yake ila akamnyoshea inspekta mkuu wa polisi Douglas Kanja kidole cha lawama kwa kutuia jicho hali hiyo.
Gachagua katika maelezo yake alisema kuwa insipekta mkuu wa polisi hakustahili kuegemea upande wowote kulinganna na hitaji la katiba kifungu 245 (b) cha katiba ambapo afisa wa polisi hafai kuegemea upande wowote anapotekeleza wajibu wake.
Gachgua aliendeleza mfulilizo wa lawama kwa inspekta mkuu wa polisi kwa kuwa mstari wa mbele kushirikiana na kuwaruhusu wahuni kumuhujumu na kuaribu mali ya thamani ya pesa nyingi ilihali vyombo vya dola vilikuwepo vikitazama tu.
Alielezea kisa cha mnamo Novemba 28, 2024 alipokuwa katika hafla ya matanga Limuru aliweza kuvamiwa na magenge ya wahuni huku thamani ya vitu vingi vikiharibiwa.
Gachagua aliendeleza msururu wa maelezo kuhusu kuvamiwa kwake katika hafla tofauti tofauti za maombi katika mikutano yake ya kisiasa.
Alisema kuwa mnamo Desemba 28,2024 akiwa katika Kaunti ya Nyandarua aliweza kurushiwa kitoza machozi mbele ya maafisa wa usalama akisema kuwa tukio hilo bila shaka lilikuwa ni tukio la kumtoa uhai.
Alipokuwa katika Kaunti ya Nyeri mnamo 18 January,2025 katika uwanja wa Kamukunji akiwa Nyeri Mchumba wake bi Doroth Gachagua aliweza kuvamiwa na genge la wahuni waliosambaratisha huduma za mkutano wa kanisa uliokuwa ukiendelea.
Mnamo 23 Machi,2025 akiwa katika kanisa la ACK Cathedral Nyeri magenge ya wahuni yalianza vurugu na hali ya wasiwasi huku wakiwakandamiza waumini .
Kutokana matokeo haya na mengine Gachagua aliazimia kumwandikia barua inspekta mkuu wa polisi Douglas Kanja kwa ajili ya kuhakikisha kuwa matakwa ya kuhakikishiwa kuwa anapewa ulinzi katika mikutnao yake ya kisiasa linatekelezwa, Serikali kupitia kwa usalama wa ndani ihakikishe kuwa familia yake inalindwa ipasavyo miongoni mwa matakwa mengine.