logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Amerika yamshutumu Rais Traore kwa kutumia rasilimali ya nchi vibaya

Marekani kupitia kwa Jenerali wake Michael Langley imesema rais Traore anajinufaisha pekee yake.

image
na Evans Omoto

Yanayojiri22 April 2025 - 10:33

Muhtasari


  • Taifa hilo limesema kuwa rais Traore anatumia  raslimali za  taifa kujinufaisha pekee yake badala ya raslimali hizo ziwasaidie wananchi.
  • Katika kiipindi cha muda  mfupi uliopita rais  Rais Traore alionekana akitangaza amri kadha ziweze kutekelezwa kwa namna moja au nyingine .
Rais wa Burkina Faso

Taifa  la Marekani kupitia kwa jenerali wake Afrika chini ya muungano wa Africom Jenerali  Michael Langley lisema Rais wa Burkina Faso Ibrahim Traore  anaharibu rasilimali za  taifa.

Taifa hilo limesema kuwa rais Traore anatumia  raslimali za  taifa kujinufaisha pekee yake badala ya raslimali hizo ziwasaidie wananchi kwa miradi ya maendeleeo.

Itakumbukwa kuwa rais huyo wa  Bukina Faso katika kipindi cha uongozi wake amekuwa  akitekeleza maendeleo mengi kwa raia wa Burkina Faso tangu achukue  hatamu za uongozi.

RaisTraore kwa siku  chache zilizopita alionekana akipindua  sera za  serikali tangulizi na  kuanzisha mkakati wa  sera zake za  serikali mpya ambazo zimeonekna  zikizaa  matunda.

 Katika kiipindi cha muda  mfupi uliopita rais  Rais Traore alionekana akitangaza amri kadha ziweze kutekelezwa kwa namna moja au nyingine .

Kwa mfano katika maamuzi yake  ya awali Traore  aliweza  kutangaza  kwa kusema kuwa  mali yote  inayopatikana  chini ya  himaya ya taifa  la  Burkina Faso ilikuwa ni mali ya watu wa  Bukina Faso na ilistahili kutumiwa  kwa manufaa ya Wabukina faso.

Traore alitangaza kuwa hamna mwananchi wa taifa hilo ambaye  atalipa ushuru wowote katika bidhaa za ununuzi.

Baada ya kutangaza hivyo hilo jambo liliweza  kuwawacha wengi wakiwa katika hali ya mshangao kwa sababu hawakuweza kuamini ni kipi ambacho kilikuwa kikijiri kwa sababu kwa mara  nyingi kuwaondolea wananchi jukumu la kulipa ushuru ilimaaanisha ulikuwa  na  viwango ambavyo  ungeweza  kujisimamie peke yako.

Hilo jambo liliwatua wengi nyoyo wakakosa kuamini ikiwa Taifa hilo litafanikisha sera hiyo ya kuwaondolea wananchi wake  jukumu la kulipa ushuru. 

Rais  huyo siku ya jumatatu 21 Aprili,2025  aliweza  kutangaza kuwa masomo yote  katika  taifa  hilo yatakuwa  ya bure kuanzia chekechea hadi chuo kikuu na uhitimu  kwa  kufahamu kuwa taifa lako limekugharamia.

 Huo ni mkakati mojawapo ambao  uliwahi kutumiwa na rais wa Libya Muamari Gaddafi ila akafariki baada ya  kuwekewa vikwazo huku sababu yake kuu ya  kuwaawa alikuwa  na sauti ya kutaka afrika tuwe na safaru moja kama bara la Afrika, Nyenzo hiyo hiyo inasukwa na Traoze ndio inafanya maadhi ya mataifa ya magharibi kuweza kuhisi vibaya  na uongozi wa Traore.

 


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved