
Aliyekuwa mbunge wa Gatundu Kusini Moses Kuria na mshauri wa serikali amejutia tabia na mienendo ya wanasiasa nchini.
Kuria katika matamshi yake kwenye X aliweza kuelezea kusikitishwa kwake na hatua ya wanasiasa nchini kuchukua mkondo mbaya wa kuwakejeli walimu nchini.
''Kuna maono mengi kuhusu jinsi ya kuangamiza taifa lakini kwa yale ambayo yanaonekana na kuwa ya mvuto mkuu ni ya wanasiasa kupanga misururu ya fomu za kuwaajiri walimu katika mikutano ya hadhara na ya umma.
Hilo ni jambo la kusikitisha sana hasahasa kwetu kama viongozi amba o tumepiitia kwa walimu ambao tuanaonekana kuwakejeli licha ya kupata manufa makuu kutoka kwao, hapo tumejishusha sana'' Mosese Kuria alieleza.
Katika siku za hivi majuzi, baadhi ya wabunge walionekana wakichukulia suala la walimu kuajiriwa kama suala la kisiasa bila kufahamu kuwa ni suala ambalo huwa chini ya tume ya kuwajiri walimu TSC Nchini.
Kulingana na usemi wa katibu mkuu wa tume ya kutetea masilahi ya walimu KNUT Bwana Collins Oyuu aliweza kuwakosoa wabunge kwa kuweka mbele masilahi yao na kuikosea heshima tume ya kuwaajiri walimu TSC kwa kulichukulia hilo swala la walimu kuajiriwa kama mchezo wa paka na panya.
Oyuu alisikitikia pakubwa mienendo na tabia ambazo zimekuwa zikichuliwa na wanasiasa kwa kutembea na fomu za kuwajiri walimu kwa kuwaamuru kupanga foleni akisema kuwa ni jambo la aibu sana.
''Inasikitisha na inaudhi kuweza kuona taasinia ya ualimu ikidharauliwa kiwango cha kuweza kuwaruhusu wanasiasa kuchekea taaluma hii muhimu kwa kushinda wakiwaamuru watu kupanga foleni katika matanga na kwa sababu ya kutaka kupata sifa na imani kutoka kwa wananchi.
Walimu wanapohitajika kuajiriwa au kupandishwa cheo hilo ni jukumu ambalo liko katika katiba ya Kenya na inastahili kuheshimiwa Ambapo ni jukumu la TSC si mtu binafsi.
Kama muungano wa walimu tungependa kulani tukio hilo la aibu ambapo wabunge tena watunga sheria wetu katika bunge la taifa wanafahamu kile ambacho kinastahili kuwa kikijiri kwa ustaarabu mkuu tena wa kisheria ifaavyo'' bwana Oyuu alieleza.
Wabunge kadhaa walionekana wakiwaeleza wananchi katika hafla za mikutano kuhusu uwezo wao wa kuwapa kandarasi za kudumu za kazi ya uaalimu bila ubaguzi wala upendeleo wowote.