
Wizara ya hali ya anga imetangaza maeneo mbalimbali ya taifa yatakayoshuhudia mabadiliko ya hali ya anga.
Kulingana na idara hiyo, Nairobi itashuhudia mvua na hatimaye viwango vichache vya jua mchana huku kiwango cha juu cha joto kikipanda kwa nyusi 27 na kushuka kwa asilimia 16.
Jijini Mombasa kutashuhudiwa viwango vya kadri vya jua mchana kutwa huku kiwango cha joto kikipanda kwa nyusi 33 na kupungua kwa nyusi 25 mtawalia.
Jijini Eldoret kutashuhudiwa vivango vya kadri vya jua mchana kutwa huku kukishuhudiwa kiwango cha juu cha joto kwa nyusi 24 huku kiwango cha chini zaidi kikiwa ni nyusi 14.
Kulingana na ripoti ya utabiri wa hali ya anga Maeneo ya Nakuru yatashuhudia viwango vya kadri vya jua mchana huku kiwango cha joto cha juu kikiwa ni 26 huku cha chini kikiwa 15.
Maeneo ya Nyeri yatashuhudia viwango vya mvua pamoja na jua mchana huku kiwango cha joto cha juu kikiwa ni 26 na cha chini kikiwa ni 15.
Maeneo ya Marsabit kulingana na ripoti ya utabiri wa hali ya anga kutashuhudiwa viwango vya mvua pamoja na joto la kadri huku kiwango cha juu sana cha joto kikiwa 25 na cha chini 15
Katika kaunti ya Kakamega kutashuhudiwa viwango vya jua la wastani mchana huku viwango vya joto vikiwa ni 28 kwa kiwango kikuu na 18 kiwango cha chini mtawalia.
Idara hiyo ya utabiri wa hali ya anga iliwataahadharisha wakenya wote kuwa makini wanaposafiri na kuwashauri kuhakikisha kuwa wanabeba na kuvalia nguo nzito wanaposafiri ili kuepuka kupatwa na maradhi ya ghafla.
Vilevile utabiri huo uliwarahihishishia na kuhakikisha kuwa wale wote waliokuwa na ratiba ya kusafiri wanajipnga kwa uzuri na kwa wakati ili kuepuka masaibu.
Hata hivyo ni afueni kwa wakulima wanaoendesha kilimo hasa cha upanzi wa mimea mbalimbali kwani kwa sasa wamebahatika kuweza kupata ratiba nzuri ya jinsi wanastahili kujipanga kwa kilimo ili kuhakikisha kuwa hamna lolote liendalo kwa ubaya.