logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Ghadhabu kufuatia visa vya ujambazi, wizi wa ng'ombe Kerio Valley

Maisha ya watu wasio na hatia yanapotezwa huku machache yakifanyiwa kudhibiti hali hiyo.

image
na Radio Jambo

Yanayojiri12 July 2022 - 06:58

Muhtasari


•Wataalamu wameeleza wasiwasi wao kuwa maisha ya watu wasio na hatia yanapotea huku machache yakifanywa kudhibiti hali hiyo.

•Mutwol alisema ni jukumu la serikali kuhakikisha maisha na mali za watu zinalindwa katika sehemu yoyote ya nchi.

Wanajeshi

Wataalamu kutoka Kerio Valley, Marakwet Mashariki, wanalalamika kuhusu ongezeko la visa vya ujambazi na wizi wa ng'ombe.

Wakiongozwa na Lawrence Mutwol, walielezea wasiwasi wao kuwa maisha ya watu wasio na hatia yalikuwa yakipotea huku machache yakifanywa kudhibiti hali hiyo.

Alieleza kwamba  Kirop Yualanyang wa kijiji cha Kowow aliuliwa  na majambazi wanaoaminika kuvuka kutoka Tiaty katika Kaunti ya Baringo.

Mutwol, ambaye anawania kiti cha ubunge cha Marakwet Mashariki kama mgombeaji huru, alisema atashinikiza kufidiwa kwa maisha yaliyopotea na mali kuharibiwa, ikiwa atachaguliwa mnamo Agosti.

"Inasikitisha kwamba maisha ya watu wasio na hatia yanapotea lakini ni shughuli kawaida kwa upande wa serikali kwani hakuna lolote wanaoifanya kuhusu swala hilo," alisema.

Akizungumza alipozuru kijiji cha Kowow, nyumbani kwa marehemu Kirop, kufariji familia iliyoachwa, Mutwol alisema atashinikiza kufidiwa kwa maisha na mali yote iliyopotea kutokana na ujambazi na wizi wa mifugo.

Aliongeza: "Kwa kweli, serikali inapaswa kusomesha watoto wa wale waliouawa na majambazi". Alisikitika kuwa viwango vya elimu vimedorora Marakwet Mashariki kwa sababu ya uongozi mbaya.

Alisema ni jukumu la serikali kuhakikisha maisha na mali za watu zinalindwa katika sehemu yoyote ya nchi, bila kujali itikadi zao za kikabila au kisiasa.

"Watu wa Marakwet wana haki ya usalama kama ilivyoainishwa katika Katiba. Sio neema bali ni haki,” alisema.

Alisikitika kuwa viwango vya elimu vimedorora sana Marakwet Mashariki kwa sababu ya uongozi mbaya, akiongeza kuwa ni jukumu la viongozi wote waliochaguliwa kuhubiri amani na maridhiano.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved