IEBC yawasilisha fomu zote za uchaguzi katika mahakama ya Milimani

Fomu hizo zitatumika kama ushahidi katika kesi ya kupinga ushindi wa Rais William Rut

Muhtasari

•IEBC mnamo Jumatano alasiri iliwasilisha fomu 34A zote kwa Mahakama ya Juu. 

Maafisa wa IEBC katika Mahakama ya Milimani mnamo Agosti 24
Maafisa wa IEBC katika Mahakama ya Milimani mnamo Agosti 24
Image: ANNETTE WAMBULWA

Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka nchini (IEBC) mnamo Jumatano alasiri iliwasilisha fomu 34A zote kwa Mahakama ya Juu. 

Fomu 34A, 34B na 34C, ambazo zilitumika kumtangaza mshindi wa uchaguzi wa Agosti 9, zitatumika kama ushahidi katika kesi ya kupinga ushindi wa Rais mteule William Ruto.

Waliokuwepo ni Mkurugenzi Mtendaji Marjan Marjan na Kamishna Boya Molu. 

Wakili Wambua Kilonzo pia yupo. 

Ni hitaji la kisheria kwa tume kutoa hati saa 48 baada ya kuwasilishwa kwa ombi.

Mahakama ya Juu inatarajiwa kusikiliza maombi tisa yaliyowasilishwa Jumatatu kupinga matokeo ya uchaguzi wa urais wa Agosti 9.

Malalamiko yana uwezekano wa kuunganishwa katika rufaa moja wakati wa mkutano wa kabla ya kesi.

Muungano wa Azimio la Umoja One Kenya pamoja na walalamishi wengine wanane wanataka Mahakama ya Juu kubatilisha ushindi wa Ruto kwa madai ya makosa na kutolingana kwa matokeo ya uchaguzi.

Ruto, Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka na mwenyekiti wake Wafula Chebukati wameorodheshwa kuwa wahusika katika kesi hizo.