Msako dhidi ya bidhaa ambazo hazijatozwa ushuru wafanyika Nyanza

Tembe za dawa ya Kamagra zilikamatwa katika maduka kadhaa ya kuuza dawa jijini Kisumu.

Muhtasari

• Polisi wafanya msako wa bidhaa zisizolipiwa kodi ya kuagizwa katika eneo pana la Nyanza kwa ushirikiano na polisi wa kimataifa.

•Bidhaa mbali mbali zinazuiliwa na polisi sawia na washukiwa kukamatwa kutokana na msako huo.

crime scene
crime scene

Kikosi cha wakala mbali mbali kwa ushirikiano na polisi wanafanya msako wa kutafuta bidhaa ambazo inadaiwa hazijalipiwa ushuru katika maduka eneo ya Nyanza.

Tayari bidhaa za urembo zikiwemo Vaseline, Dove na St. Ives kutoka duka la Best Ladies zinazuiliwa na maafisa hao.

Mshukiwa mmoja pia kwa jina Brian Ouya alikamatwa na sasa anawasaidia polisi na ujasusi zaidi

Dawa hizo za Kamagra pia zilipatikana katika duka la dawa la Victoria na washukiwa wanne walikamatwa.

Kikosi hicho cha jina la Operation Usalama X, kilifanya msako katika maduka mengine katika mji wa Kisumu na kunasa washukiwa hata zaidi.

Katika duka la dawa la Leo kwenye barabara ya Kisumu kuelekea Kakamega. maafissa hao walinasa tembe za dawa ya Kamagra na oral jelly  ambazo zilikuwa hazijalipiwa ushuru wa kuagiza kati ya bidhaa nyingine.

Vile vile, polisi wanamzuilia mmiliki wa duka la jumla kwa jina Abdulrehman Mohamed Yasheen aliyepatikana na mikebe ya PVC-U na soda flakes ambazo zinaaminika kuwa hazijalipiwa kodi ya kuagizwa nchini. 

Kikosi cha Operation Usalama X kinaongozwa na ushirikiano wa wakuu wa polisi Afrika mashariki (EAPCCO)  wenye wanachama 14.

EAPCCO inashirikiana na shirika la muungano wa wakuu wa police ukanda wa Afrika kusini (SARPCCO)  unaolenga kuzuia na kupigana na uhalifu wa kimataifa uliopangwa.

Operasheni ya miungano hii miwili inafanya kutokana na ongezeko la visa vya wizi wa magari, biashara ya watu, utoroshaji wa madini na uuzaji wa silaha baina ya nchi.