logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Mume asakwa baada ya mwili wa mkewe uliokuwa unaoza kupatikana nyumbani kwake

Kwa mujibu wa polisi, kichwa kilikuwa kimefungwa kabisa na shuka na kufungwa vizuri shingoni huku damu ikitoka puani.

image
na Samuel Maina

Habari23 August 2024 - 07:59

Muhtasari


  • •Hakuwa ameripoti kazini tangu Jumatatu na ni hadi siku ya Jumatano usiku ambapo mwili wake uligunduliwa.
  • •Kwa mujibu wa polisi, kichwa kilikuwa kimefungwa kabisa na shuka na kufungwa vizuri shingoni huku damu ikitoka puani.

Maafisa wa upelelezi wanamsaka mwanamume anayeshukiwa kumuua mkewe katika soko la Ogwedhi, Kaunti ya Migori.

Mwili uliokuwa ukioza wa Jackline Pilli, 31 ulipatikana kitandani mwake siku chache baada ya kutoweka.

Hakuwa ameripoti kazini tangu Jumatatu na ni hadi siku ya Jumatano usiku ambapo mwili wake uligunduliwa.

Polisi wanashuku kuwa aliuawa Jumapili usiku na mwili ukaachwa katika eneo la tukio.

Dada wa marehemu alifahamisha polisi kuwa shemeji yake alimpigia simu akidai marehemu alikuwa mgonjwa na hali yake ni mbaya.

Alipompigia ili kuthibitisha mahali alipo dada huyo, aligundua kuwa simu ya mkononi ilikuwa imezimwa.

Alienda katika soko la Ogwedhi ambako dadake alikuwa akiendesha biashara ya hoteli na alifahamishwa na wafanyakazi wa pale dadake alionekana mara ya mwisho katika kituo hicho Jumatatu, Agosti 19 asubuhi.

Jackline inasemekana aliondoka mahali hapo akisema anaenda nyumbani kutatua mzozo wa kifamilia na mumewe.

Walikuwa watu pekee ndani ya nyumba wakati huo.

Dada huyo na wafanyakazi wengine wa pale hotelini walikwenda kwenye nyumba hiyo na kukuta imefungwa kwa nje na kuwafanya kutafuta usaidizi wa polisi ili kufungua.

Mwili wa mwanamke huyo ulipatikana ukiwa chini karibu na kitanda chake.

Kwa mujibu wa polisi, kichwa kilikuwa kimefungwa kabisa na shuka na kufungwa vizuri shingoni huku damu ikitoka puani.

Mwili ulikuwa ukioza wakati huo. Uliondolewa na kupelekwa katika hifadhi ya maiti ya Hospitali ya Rufaa ya Kaunti ya Migori ikisubiri kufanyiwa uchunguzi.

Polisi walisema wanamsaka mshukiwa anayejulikana kuhusiana na mauaji hayo ili kubaini sababu na kuchukua.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved