Mwanamke amdunga mpenziwe kwenye mapaja, sehemu za siri kisha kujisalimisha kwa polisi Kirinyaga

Polisi wanamzuilia mshukiwa kwa ajili ya mahojiano huku uchunguzi zaidi ukusubiri kufanyiwa.

Muhtasari

•Mwanamke wa miaka 38 anazuiliwa katika kituo cha Kagio kwa madai ya kumuua mpenzi wake mjini Kagio.

•Mshukiwa na marehemu walikuwa wanaishi pamoja kwenye chumba cha kukodi mjini Kagio.

Crime scene
Crime scene
Image: HISANI

Mwanamke mmoja mwenye umri wa miaka 38 anazuiliwa katika kituo cha Kagio kwa madai ya kumuua mpenzi wake mjini Kagio.

Mshukiwa anaripotiwa kumdunga mpenziwe mara tano, kwenye mapaja na kwenye kwenye sehemu zake za siri na kupelekea kifo chake.

Wakati akithibitisha tukio hilo, bosi wa polisi wa eneo la Kirinyaga Mashariki Moses Koskei alisema mwanadada huyo ambaye anafanya kazi katika baa moja mjini Kagio alijisalimisha mikononi mwa polisi baada ya kutekeleza unyama huo.

“Alimdunga mpenzi wake mara tano, mara mbili kwenye paja la kushoto, two times kwenye paja la kulia na kwenye sehemu zake za siri,” Koskei alisema.

Koskei alisema mpenzi wa mshukiwa aliaga baada ya kupoteza damu nyingi mwilini kutokana na majeraha ya kisu. Aidha, alithibitisha kuwa bado hawajafanikiwa kupata kisu ambacho kilitumika kutekeleza mauaji.

Mshukiwa na marehemu walikuwa wanaishi pamoja kwenye chumba cha kukodi mjini Kagio. Haijabainishwa ni nini kilipelekea mauaji hayo. Haijabainishwa ni nini kilipelekea mauaji hayo.

Polisi wanamzuilia mshukiwa kwa ajili ya mahojiano huku uchunguzi zaidi ukusubiri kufanyiwa.

Mwili wa marehemu umehifadhiwa katika chumba cha kuhifadhi maiti cha hospitali ya rufaa ya Kerugoya.