Ruto avunja kimya kuhusu kuondolewa kwa mihula ya rais

Rais amewaambia wabunge wa UDA kuwa hana nia ya kubadilisha katiba ili kuondoa mihula ya rais.

Muhtasari

• Rais alisema wabunge hao wanapaswa kutanguliza miswada ambayo itaboresha maisha ya Wakenya.

•Aliongeza kuwa lengo lake pekee kwa sasa ni kuwafanyia kazi watu wa Kenya.

DP RUTO WAKATI WA MANIFESTO YA KENYA KWANZA 30 JUNI 2022
Image: EZEKIEL AMING'A

Rais William Ruto amewaambia wabunge wa UDA kuwa hana nia ya kubadilisha katiba ili kuondoa  mihula ya rais.

Akizungumza Jumatano, Rais alisema wabunge hao wanapaswa kutanguliza miswada ambayo itaboresha maisha ya Wakenya.

Aliongeza kuwa lengo lake pekee kwa sasa ni kuwafanyia kazi watu wa Kenya.

"Msitumie muda wenu kushinikiza sheria za ubinafsi, kama vile kubadilisha Katiba ili kuondoa mihula ya rais, lengo langu ni kuwatumikia wananchi," Ruto alisema.

Aliyasema hayo Jumatano asubuhi alipokuwa akiongoza kikao cha Wabunge wa UDA kwenye Ikulu.

Siku chache zilizopita, mbunge wa Fafi Salah Yakub aligonga vichwa vya habari baada ya kutoa matamshi ya kutaka kuondolewa kwa mihula ya rais.

Yakub katika pendekezo lake alisema umri ndio unapaswa kuzingatiwa umri na sio huduma ya muda.

Mbunge huyo wa UDA alidai kuwa baadhi ya wabunge wenzake tayari wanafanyia kazi muswada wa marekebisho ya Katiba ili kubadilisha mihula miwili rais na kuweka kizuizi kuwa umri wa miaka 75.

Mbunge huyo alitoa mfano wa marehemu Rais Mwai Kibaki ambaye alistaafu baada ya mihula miwili ya miaka mitano licha ya kile alichosema kuwa utendakazi wake bora uliogeuza uchumi wa nchi.

“Nadhani tulifanya makosa kumruhusu aende nyumbani baada ya kumaliza muda wake. Tulipunguza ndoto yake wakati Katiba ilipomwondoa lakini alihudumu vyema katika mihula miwili,” Yakub alisema.

tungeweza kufikia hadhi ya Malaysia au Singapore. Je, ni vyema kumwondoa mtu kwa sababu muda wake umefika mwisho na bado anafanya kazi,” alisema.

Chama cha Rais William Ruto, UDA hata hivyo kilikanusha mipango ya kubadilisha Katiba ili kuondoa ukomo wa mihula ya urais.

Kwa niaba ya chama, Mwenyekiti Johnson Muthama alisema hawahusiki katika mazungumzo ya kuondoa mihula au kuweka kikomo cha umri.

“Mheshimiwa Yakub alitoa kauli binafsi ambayo haina uhusiano wowote na UDA. Kama chama, tunasimamia demokrasia iliyo wazi na tunasalia kuunga mkono ukomo wa urais wa mihula miwili na hakuna majadiliano yanayoendelea ya kuufuta,” Muthama alisema.