(Video) "Hatutaki uchaguzi!" Jamaa asababisha drama kwenye mkutano wa IEBC

"Kilichofanyika Sri Lanka kitatokea Kenya...tunataka haki na usawa..." Alisema.

Muhtasari

•Jamaa huyo alionekana kuandamana pekee yake kwani hakuna waandamanaji wengine walioonekana katika eneo la tukio.

Mwanamume mmoja alifurushwa na na maafisa wa polisi baada ya kujaribu kuandaa maandamano wakati wa Kongamano la Kitaifa la Uchaguzi la Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) katika ukumbi wa KICC jijini Nairobi. 

"Hatutaki uchaguzi katika nchi hii, tunataka usawa. Tunataka uhuru," Jamaa huyo alisikika akisema huku akiwa ameinuliwa juu juu na maafisa watatu.

Jamaa huyo hata hivyo alionekana kuandamana pekee yake kwani hakuna waandamanaji wengine walioonekana katika eneo la tukio

"Kilichofanyika Sri Lanka kitatokea Kenya...tunataka haki na usawa..."  Alisema.

Jumamosi maelfu ya waandamanaji Sri Lanka walivamia makazi rasmi ya waziri mkuu na kuchoma moto nyumba yake.

Waandamanaji hao walimtaka waziri mkuu na rais wa nchi hiyo ajiuzulu  huku wakiapa kutoondoka pale hadi agizo lao litimie.

Tukio hilo limezua mjadala mkubwa kote duniani huku baadhi ya Wakenya wakionekana kukejeli hatua hiyo na wengine wakiwaunga mkono WaSri Lanka.